Thursday, 26 February 2015

TAHARUKI YATANDA HUKO KHARKIV ..>>

 Waandamanaji washikilia bango la kuunga mkono Kikosi cha "Azov" wakati wa maandamano ya Februari 22 mjini Kharkiv.

kwa wakati huu, makubaliano ya usitishwaji mapigano yametekelezwa mashariki mwa Ukraine.

Lakini katika mji wa Kharkiv, ambao ni mji wa pili wa Ukraine, hali ya taharuki imeendelea kutanda baada ya shambulio la bomu lililogharimu maisha ya watu wanne wakati wamaandamano ya amani Jumapili Februari 22. Hali ya vurugu inahofiwa kutokea kwa wakati wowote mjini humo.

Kusini mwa Ukraine, kwenye uwanja wa mapigano, kumekua na wasiwasi kwamba mji wa Marioupol unaweza kulengwa na waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la Ukraine.

Kwa mujibu wa wanahabari wa RFI mashariki mwa Ukraine, Sébastien Gobert na Régis Gente, wakazi wa Kharkiv wanaishi kwa hofu ya kutokea kwa vita tangu miezi miwili iliopita, kufuatia kuonekana kwa misafara ya magari ya kijeshi pamoja na kuwasili kwa wakimbizi na watu walioathirika na mapigano mashariki mwa Ukraine.

Mwanasheria Nataliya Okhotnik, mjumbe wa shirika la kulinda haki za binadamu, amekumbusha kwamba bomu la Februari 22 ni miongoni mwa mfululizo wa milipuko ya miezi ya hivi karibuni. Lakini ni kwa mara ya kwanza milipuko hio inasababisha maafa.

No comments:

Post a Comment