Watu 36 waliuawa katika mji mdogo wa Niger wa Abadam, unaopakana na Nigeria, kwenye umbali wa kilomita zaidi ya kumi na mbili, na wengine zaidi ya ishirini walijeruhiwa katika shambulio la bomu lilioendeshwa na ndege isiyojulikana
Watu hao walikua katika sherehe za mazishi katika Msikiti mmoja wa mji huo wa Abadam.Abadam ni kijiji kinachopatikana kwenye mpaka na Nigeria. Sehemu mmoja ya Abadam upande wa Nigeria ilikua ikikaliwa na wanamgambo wa Boko Haram, miezi kadhaa iliyopita.
Hata hivyo wakazi wa sehemu hiyo wamekua wakitiwa hofu na hali hio inapofika usiku, wengi wamekua wakilala msituni, na wanarejea inapofika asubuhi.
Ndege isiyojulikana ilishambulia Msikiti mmoja wa kijiji hicho Jumanne wiki hii, wakati walikua katika sherehe za mazishi, upande wa Niger.
Zaidi ya watu 30 walikua katika Msikiti wakitoa hashimu za mwisho kwa mzee mmoja aliyefariki siku tatu zilizopita.
Kwa mujibu wa shahidi mmoja aliye kuwa eneo la tukio, Msikiti umeteketezwa ikiwa ni pamoja na nyumba ziliyokua pembezoni mwa Msikiti huo.
Shambulio hilo liligharimu maisha ya watu wengi, wakiwemo wanawake na watoto ambao walikua ndani ya nyumba hizo. Mkuu wa kijiji na wawili kati ya watoto zake waliuawa katika shambulio hilo.
Shahidi huyo, amebaini kwamba aliona ndege mbili zikipaa eneo la tukio. Ndege moja ilirusha mabomu mawili kwenye umbali wa zaidi ya mita mia moja na kijiji cha Abadam, ndege nyingine ilirusha bomu kwenye Msikiti.
Nigeria iliendesha shambulio dhidi ya wapiganaji wa Boko Haram waliokua eneo hilo tangu miezi minne iliyopita.
No comments:
Post a Comment