Wednesday, 25 February 2015

MANCHESTER CITY YABURUZWA HOME ...>> 2-1

 
Manchester City imefungwa mabao 2-1 katika mchuano wake na Barcelona wakati ilikua ikichezea nyumbani Jumanne jioni Februari 24.

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Luis Suarez alikua na bahati ya kipekee baada ya kuiwezesha timu yake mpya ya Barcelona kupata ushindi wa mabao mawili 2-1 dhidi ya Manchester City katika mechi ya Klabu Bingwa barani Ulaya .

Suarez amefunga mabao yote mawili na hivyo kuwashangaza mashabiki wa Manchester City.
Goli pekee la kufutia machozi la Manchester City lilitiwa kimiani na mshambuliaji wa timu hiyo Sergio Aguero. Hadi dakika 90 za mchezo Manchester City wakiwa nyumbani walijikuta wakiburuzwa na Barcelona kwa mabao mawili kwa moja lao la kufuta machozi.

Na katika mechi nyingine ya michuano klabu bingwa barani Ulaya, Juventus ya Italia wakiwa nyumbani waliwaadhibu Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa mabao mawili kwa moja.

Magoli ya Juventus yalitiwa kimiani na Carlos Tevez na Alvaro Morata, huku bao la Borussia Dortmund likitiwa kimiani na Marco Reus.

No comments:

Post a Comment