Friday, 20 February 2015

POWER OF MEDIA .. MAMIA KWA MAELFU WATANDA BARA BARANI BURUNDI ..>>>

 
Mkurugenzi wa radio, RPA, inayosikilizwa na raia wengi nchi Burundi na baadhi ya maeneo ya nchi jirani ameachiwa huru kwa dhama Jumatano februari 18, lakini ameruhusiwa kutoka jela Alhamisi wiki hii.

Bob Rugurika bado anakabiliwa na tuhuma za kushirikiana na kundi la wahalifu katika mauaji ya watawa watatu kutoka Italia waliouawa mwezi Septemba mwaka 2014 wilayani Kamenge mjini Bujumbura.

Hata hivyo waandamanaji wanadai kuachiliwa huru kwa Christian Butoyi, mtu aliyekamatwa na polisi na kuzuiliwa katika jela kuu la Mpimba, mjini Bujumbura, akituhumiwa kuhusika katika mauaji hayo. Mtu huyo anadaiwa kuwa na maradhi ya akili.

Picha ya Christian Butoyi, mwenye umri wa mika 33, anaedaiwa kuwaua watawa watatu kutoka Italia, wakati akionyeshwa na polisi mbele ya vyombo vya habari mjiniBujumbura, Septemba 9 mwaka 2014.
 
RFI/Esdras Ndikumana
Waandamanaji wamekua wakibebelea matawi ya miti wakidhihirisha furaha yao. Baada ya mkurugenzi wa redio RPA kupokelewa kwa changwe, vifijo na nderemo kwenye makao makuu ya redio RPA, mjini Bujumbura, polisi ililazimika kutumia nguvu kwa kuwatawanya waandamanaji. Hadi saa tano mchana Alhamisi wiki hii, hali ya sintofahamu ilikua ikiendelea katika mji wa Bujumbura.

Mahakama ya rufaa katika manispaa ya jiji la Bujumbura, nchini Burundi, imemuachilia huru mkurugenzi wa redio RPA, Bob Rugurika, kwa dhamana ya pesa za Burundi milioni 15, sawa na dola za kimarekani elfu 10.
Kwa sasa mkurugenzi wa redio RPA ataendelea kusikilizwa mahakamani akiwa huru.
tags: Burundi - Pierre Nkurunziza

No comments:

Post a Comment