Rais wa Liberia Ellen Johnson
Sirleaf anasema kuwa mipaka ya nchi yake itafunguliwa kesho Jumapili
baada ya kufungwa mwaka uliopita kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa
ebola.
Alisema kuwa serikali itahakikisha kuwa hatua zimewekwa kuzuia ugonjwa wa ebola kuingia nchini humo kupitia kwa vifuko vyote vya mipaka ya nchi hiyo.
Liberia ni moja ya nchi tatu za Afrika magharibi kati ya Sierra Leone na Guinea iliyoathirika vibaya na ugonjwa wa ebola lakini hatahivyo imefanikiwa kuudhibiti ugonjwa huo
Ugonjwa wa ebola umewaua zaidi ya watu 9000 magaharibi mwa Afrika.
No comments:
Post a Comment