Monday, 23 February 2015

BARA BARA ZA TANZANIA NI SAWA NA SIMU YA MCHINA ..>>


Natanguliza sala kabla sijaongelea ya moyoni kuzihusu bara bara za nchi yangu zilizotumia kodi yangu na kuamuliwa na watumishi wangu kuzikarabati na kuzijenga .

SALA ..

Baba mungu wa majeshi , nakuomba baba unipe nguvu na ujasiri baba niweze KUSHINDA BABA ,, hata wanapokuja kuniteka BABA washindwe na kulegea miguu yao , washindwe na kulegea mikono yao BABA , wadhoofishe bwana zile silaha wanazotumia kutolea kucha wazisahau nyumbani BWANA , zile za kutoboa macho nazitiisha kwa jina lako bwana , wasikate kidole ili niendelee kuandika bwana , na hata wanapoamua kunitupa bwaana  ! Wasinitupe mabwepande Bwanaa.. wasinitupe PUGU Baba .. WAKANITUPE  B.O.T bwana ,, ee bwana bariki taifa lako .. na vijana wako AMIN.

BARA BARA ZA TANZANIA KUA KAMA SIMU YA KICHINA .

Najua wengi tumeona mkeka kwenye mija yetu .. yes! ni jambo zuri sana kua na bara bara za lami kuinganisha nchi nzima saafi sana .
ILA wapaswa kujiuliza ... bara bara hizi ni za kudumu muda gani ???? 

Kwa tunaojua kupata michongo lazima utoboke sawa .. ila michongo itakayopita utaifaidi kwa muda gani kulingana na pesa uliyotoa ?? au itakua kama simu ya mchina .. marembo meengi mbwe mbwe tele ila haimalizi mwezi .. chaaali ...

Kuhusu bara bara za Tanzania kuna mengi tunayaona mfano ile bara bara inayokwenda kwa SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA BI. ANNE MAKINDA haijamaliza miaka miwili hata mmoja na nusu bado nadhani .. ila leo hii ni makorongo ... imelimwa tena .. tujiulize atakaye rekebisha upya pale ni mkandarasi mpya au yule yule ?? na atalipwa na nani kama ni mpya ??? na kama ni yule yule how can u trust him ??? unamwamini vipi kua hatozengua tena kwani nini kilimpata hata atengenize bara bara kama cm ya mchina mara ya kwanza ??
je mapambo na mbwe mbwe za bara bara zetu ni za kudumu muda gani kama wakiwa bado katika ujenzi kwingine kunabomoka .. gademn .... t'  inaudhiii ....

oyaa ... badae ..!

No comments:

Post a Comment