Kwa mujibu wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa unaohudumia watoto (Unicef), idadi ya vijana waliotekwa nyara inaweza kuongezeka.
Makundi hasimu yamekua yakitumia watoto vitani tangu mwanzoni mwa machafuko, mwezi Desemba mwaka 2013. Baadhi ya vijana waliotekwa nyara wana umri wa miaka 13. Mpaka sasa haijulikani wapi watoto hao wamepelekwa na ni kundi gani ambalo limehusika na kitendo hicho.
Hivi karibuni waasi nchini Sudan Kusini waliwaachilia huru watoto 280 ambao walikuwa walisajiliwa kujiunga nao.
Awali Mfuko wa Umoja wa Mataifa unaohudumia watoto (Unicef), ulidhibitisha kuachiliwa huru kwa watoto hao lakini ulisema bado kuna zaidi ya watoto 3,000 ambao bado wapo msituni na wanaendelea kupigana.
Inaelezwa kuwa watoto hao ambao baadhi yao wana umri wa miaka kati ya 11 na 18 wamekuwa wakipigana kwa muda wa miaka minne sasa, na hawajawahi kwenda shule na sasa kazi kubwa ni kuwabadilisha.
Wakati huo Unicef ilikua na matumaini ya kuachiliwa huru watoto wengine katika siku zijazo.
Mwakilishi wa Unicef Sudan Kusini, Jonathan Veitch alisema wakati huo, kuachiwa huru kwa kundi hilo la watoto ni hatua ya kwanza ya matumaini.
Umoja wa Mataifa unasema watoto takriban 12,000 waliandikishwa na kushirikishwa vitani mwaka 2014 nchini Sudani kusini.
Kundi la watoto walioachiwa huru mwishoni mwa mwezi Januari mwaka 2015 ni sehemu ya jeshi la waasi linaloongozwa na David Yau Yau, ambaye alisaini mkataba wa amani na serikali mwaka mmoja uliopita.
No comments:
Post a Comment