Friday, 27 February 2015

NILIKUA TAYARI KWA ADHABU YOYOTE .. KESI YANGU IMENIFUNZA MENGI .. CHIDI AKALISHWA

  

Rapper Chidi Benz kwa sasa ni mtu huru baada ya Alhamis hii kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi laki tisa. Amelipa faini hiyo.
Akizungumza leo kwenye ‘You Heard’ ya Clouds FM, Chidi amesema amejifunza mengi kupitia kesi hiyo.

“Nimejifunza kwa sababu kuna maisha halisi ambayo nimeishi kati hapo na matatizo. Ni maisha ambayo yamebadilisha sehemu kubwa sana ya maisha yangu,” amesema Chidi. “Kwanza watu wote wanafahamu tukio hili lilinitokea na nimemalizana nalo. Pia sijaisumbua mahakama, nilikubali kwamba ni kweli nimekutwa na hivyo vitu na ni kweli nilikutwa navyo na nikikataa ni sawa sawa na ujinga kwamba adhabu ni lazima nitapewa tu. Nilikuwa nipo tayari kwa adhabu yoyote,” ameongeza.

“Unajua mimi nimefanya tukio ambalo limeonekana ni tatizo kubwa sana kutokana na unajua sisi tunaishi na maadui kuna maadui wengine wanatengeneza suala lako kuonekana kubwa sana. Kwahiyo hakimu kaangalia huyu amekosea na amekubali anaweza akawa mfano kwa wengine. Kwahiyo watu wengine wajifunze na wajiweke sawa na wasafiri.”

Chidi amedai kuwa ni mama yake ndiye aliyeilipa faini hiyo.

“Mama yangu mzazi na rafiki yangu siwezi kumtaja, watu wawili tu ndo walikuwa pamoja na mimi. Mama yangu mzazi ameshughulikia kila kitu, faini pesa kulipa kila kitu kafanya yeye mama yangu mzazi. Kwahiyo mama yangu mzazi pekee ameshughulikia, namshukuru sana.”

No comments:

Post a Comment