Wa kwanza mwanaume hapo ni mimi na anaefuata anaitwa bi. Sofy ...
na mama yake na Jackson ...
Mama huyu ni mjane na ameachiwa watoto wawili mmoja anaitwa Jackson na mwingine Baazunga ambae kwa sasa yupo mtaani anabangaiza ..
Mama huyu analea familia yake kwa kazi ya kupasua mawe kwa mikono ( kuponda kokoto) , hana kinga yoyote ile na pia hana msaada wowote ule na hivyo kazi yake ndio tegemeo lake ... ujira kwa ndoo moja iliyogongwa tayari atalipwa shilingi Mia mbili za ki tanzania,.
Nauli kwenda na kurudi anapoishi mama huyu ni shilling 2,000/- ndoo kumi za kokoto hizo ni nauli tu bado kula na mengine.
Ila kwa uvumilivu wa ajabu ... huyu mama JACKSON ameifanya kazi hii kwa miaka 13 na zaidi .
Ameweza kumsomesha mwanae mmoja na sasa yupo chuo kikuu ..
Kwa muda woote huo amemsomesha mwanae JACKSON na amemlea kwa maana ya kuwatunza Jackson na mdogo wake mpaka hivi leo ... inasikitisha sana ...
duh nitaendelea. ..
Huyu ni bi. Fatma amekimbiwa na mume na ameachiwa watoto wawili na hajui lini atamuona baba yao , yaani baby wake ... Na yenye anaponda kokoto ili wanae wale .. Aliila machozi kusimulia kisa chake .. utakisoma hapa hapa .
No comments:
Post a Comment