Thursday, 26 February 2015

TAMBWE NIYOZIMA WAZUIWA BOTSWANA .... >> MWANANCHI







      
Garbrone.

 Andrey Coutinho ana bahati, hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya Amissi Tambwe, Kpah Sherman, Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite kuzuiwa kwa saa moja kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Seretse Khama, mjini Gaborone, Botswana.
Mbrazili Coutinho hakuondoka na wenzake kutokana na kuwa majeruhi wa goti aliloumia katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City mwishoni mwa wiki.
Yanga iliwasili Gaborone saa 4: 35 asubuhi (5:35 kwa saa za Tanzania) na kukutana na kadhia hiyo baada ya wachezaji wake kulazimika kukaa hapo kwa zaidi ya saa wakisubiri suala la wenzao kukamilisha taratibu za uhamiaji.
Wakati wachezaji wakipita katika ukaguzi wa pasi za kusafiria, zile za nyota hao wa kigeni zilionekana na dosari ndogo ambazo uongozi wa Yanga umetamka kwamba walifichwa wakati wakiulizia mambo ya muhimu kuhusu safari yao.
Maofisa hao wa usalama walianza kumzuia Mrundi Tambwe akifuatiwa na Mliberia, Sherman kabla ya kuhamia kwa Wanyarwanda, Twite na Niyonzima.
Maofisa hao walidai kuwa raia hao wa kigeni walitakiwa kuwa na viza za kuingilia nchini humo hati ambazo zilikuwa na msamaha kwa wachezaji na viongozi Watanzania pamoja na kocha Mholanzi, Hans Pluijm.
Kutokana na hali hiyo, mkuu wa msafara wa Yanga kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ayoub Nyenzi akiwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tibohora walimwaga fedha kuwaondoa wachezaji hao katika kizuizi. Akizungumzia hali hiyo, Tiboroha alisema walishangazwa na hatua hiyo ya wachezaji wao kuzuiwa kutokana na awali wakati wanapata taarifa ya nyaraka wanazotakiwa kukamilisha hawakuambiwa kuhusu hayo.
“Hizi ni siasa za mpira, Yanga tumeshangazwa na hili tuliuliza mapema kule katika ofisi zao za ubalozi wa Botswana jijini Dar es Salaam hatukuambiwa kama kuna hili la viza tunatakiwa kulifanya.
Hata wao wakati tunawapokea kule kwetu walikuwa na wachezaji wageni kutoka Zimbambwe, hawakufanyiwa haya, tumelazimika kutoa fedha nyingi ili kuwaondoa wachezaji wetu pale uwanjani,” alisema Tiboroha.
Yagomea basi, hoteli
Katika hatua nyingine, Yanga ikiongozwa na makamu mwenyekiti wake, Clement Sanga iligomea basi na hoteli waliyoandalizi wa wenyeji wao, BDF XI kwa kuhofia hujuma.
Sanga ameliambia gazeti hili kuwa jambo la kwanza ambalo uongozi wao uliligomea baada ya kujiridhisha ni hoteli isiyokidhi viwango vya timu yao ambapo wanajeshi hao walipanga timu ifikie katika eneo lisilokuwa na utulivu wa kutosha.

No comments:

Post a Comment