Watu 400,000 wameshiriki katika maandamano baridi Jumatano jioni wiki hii kwa kutoa heshima za mwisho kwa Mwendesha mashitaka Alberto Nisman, aliyefariki mwezi mmoja uliyopita.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari katika mji wa Buenos Aires, Jean-Louis Buchet, Mwendesha mashitaka huyo alifariki nyumbani kwake katika mazingira ya kutatanisha, ambapo uchunguzi haujaweka wazi sababu za kifo chake.
Nisman alimtuhumu, kabla ya kifo chake, rais wa Argentina, Cristina Kirchner kwa kutaka kumuachilia huru raia mmoja wa Iran aliyefunguliwa mashitaka kwa tuhuma za kuhusika katika shambulio dhidi ya kampuni Amia inayomilikiwa na Myahudi, shambulio ambalo liligharimu maisha ya watu 85 mwaka 1994.
Avec notre correspondant à Buenos Aires,Jean-Louis Buchet
Waandamanaji hao ambao walikusanyika kwenye eneo la Mei wakati walipopita mbele ya jengo la ofisi alipokua akifanyia kazi Alberto Nisman, walikua wakilalamika “haki”.
“ Tabia ya kutowaadhibu wahalifu imekithiri, watu hawasikilizwi, watu hawatendewi haki. Lakini ni matumani kwamba ukweli utajulikana kuhusu kesi ya mwendesha mashitaka huyo”, amesema Camila, mwanafunzi wa chuo kikuu, mwenye umri wa miaka 22.
Alberto, daktari mwenye umri wa miaka 50, amesema hana imani na vyombo vya sheria vya Argentina, na amekata tamaa kuhusu uchunguzi wa kifo cha Nisman.
" Mimi niko hapa, kwanza kutoa heshima za mwisho kwa marehemu lakini pia kusema kwamba nimechoshwa na hali hii, na nina mashaka kuhusu uchunguzi wa kesi yake'', amesema daktari huyo.
Kulingana na tafiti, 80% ya raia wa Argentina wanaamini kwamba Nisman aliuawa, wakati ambapo, kulingana na uchunguzi unaoendelea, kuna uwezekano kuwa Mwendesha mashitaka huyo alijiua.
No comments:
Post a Comment