Mashahidi wanasema kundi la wanamgambo wa Boko Haram wa nchini Nigeria lilishambulia mji mmoja huko Niger Ijumaa.
Shambulizi hilo linakuwa ni lapili la kukatisha mpaka kufanywa na kundi hilo kwa wiki hii.
Wakazi wa mji wa Bosso, wapatao 50,000 uliopo kusini mwa mpaka wa Niger, waliripoti kusikia milipuko na milio ya risasi wakati wapiganaji wa ki-Islam wenye msimamo mkali walipovamia mji huo.
Shirika la habari la Associated Press limemkariri mkazi mmoja wa Bosso akisema wapiganaji waliondoka baada ya mapambano ya muda wa saa nzima na wanajeshi.
Haikuwa wazi kama wanamgambo walikuwa wakipambana na majeshi ya usalama ya Niger au wanajeshi kutoka Chad, ambayo imeweka mamia ya wanajeshi huko Bosso hapo Jumanne.
Waziri wa ulinzi wa Cameroon, amesema kwamba kiasi cha raia 91, wanajeshi 13 wa Chad na wanajeshi sita wa Cameroon waliuwawa pamoja na idadi isiyojulikana ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
No comments:
Post a Comment