Wednesday, 18 February 2015

HATUPIGANI NA UISLAM ...''OBAMA''

 Rais  Barack Obama akizungumza huko White House katika mkutano maalum uliolenga kupambana na itikadi za msimamo mkali, Feb. 18, 2015 huko Washington.
Rais wa Marekani Barack Obama amewasihi viongozi wa makundi ya  kiraia na kidini duniani kote kuungana katika mapambano dhidi ya kile alichokiita “ahadi za uongo za wenye msimamo mkali” na kupinga dhana kwamba magaidi wanawakilisha Uislam.

Katika mkutano  Jumatano jijini Washington uliolenga kupambana na itikadi za msimamo mkali, bw. Obama alisema wenye msimamo mkali , “wanajaribu kujionyesha kama viongozi  wa kidini na mashujaa wa kidini.” Obama alisema watu hao si viongozi wa kidini, ni magaidi.

Rais huyo wa Marekani aliendelea kusema “hatuna vita na Uislam, tuko vitani na watu waliokufuru Uislam.”
 Aliuwambia mkutano huo wa siku tatu kwamba pambano dhidi ya watu wenye msimamo mkali  halitaweza kufanikiwa kwa nguvu za kijeshi pekee. Alitoa mwito wa moja kwa moja kwa viongozi wa Kiislam kupinga  wale wenye msimamo mkali na kuwataka  wazungumze kwa sauti  kuondoa dhana kwamba kuna nchi ambazo zinapinga Uislam

No comments:

Post a Comment