Monday, 16 February 2015

KABLA AWATOSA UN ... >>

 
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lilizindua Alhamisi Januari 29 mwaka 2015 shughuli za kijeshi "Sokola2" ili kupokonya silaha waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR. MONUSCO ilikaribishwa uamuzi huo na kutangaza kwamba itatoa msaada wa vifaa kwa jeshi
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo amesema akisisitiza mbele ya mabalozi 21 wa jumuiya ya kimataifa nchini humo, ikiwa ni pamoja na mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, kwamba nchi yake haihitaji tena msaada wa Umoja huo ili kupambana na waasi wa FDLR.

Katika mkutano ambao haukuashiria hali ya mazungumzo ya kawaida, Rais Kabila amekosoa tabia ya mabalozi hao kuingilia masuala ya ndani ya nchi huku akitangaza kutohitaji tena msaada wowote wa kijeshi kutoka kwa askari wa kulinda amani nchini humo MONUSCO.

Juma lililopita, Ujumbe wa umoja wa mataifa MONUSCO umetangaza kwa upande wake kusitisha msaada wowowte wa kijeshi kupambana na waasi hao ili kupinga uteuzi wa majenerali wawili wanaotuhumiwa kutekeleza vitendo vya uhalifu nchini humo, tuhuma ambazo zinaendelea kutipiliwa mbali na serikali ya Congo.

Hatua ya kukataa msaada wa Umoja wa Mataifa inaweza kuwa njia moja wapo ya kutoanzisha operesheni halisi dhidi ya waasi wa FDLR iliyotangazwa kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi Januari na ambayo hadi sasa haijatekelezwa kulingana na vyanzo tofauti.

Kufwatia msimamo huo wa serikali ya rais Kabila, MONUSCO itakuwa kwenye nafasi ngumu ambapo mamlaka yake inahitaji kukabiliana na waasi wa Kihutu wa Rwanda, na ambapo serikali ya Congo inajikuta kubanwa na mamlaka hiyo ya Umoja wa Mataifa nchini humo baada ya kuridhia msaada wa Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment