Mpatanishi wa IGAD Seyoum Mesfin alionya
kuwa yeyote atakayevunja makubaliano yaliyotiwa saini hivi karibuni, ataripotiwa
kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na
kamanda wa waasi Riek Machar wamesaini makubaliano ya kumaliza mzozo ambao
umegubika na kuharibu nchi yao.
Makubaliano hayo ya kusitisha
mapigano yalitiwa saini Jumatatu mjini Addis Ababa Ethiopia kwa msaada wa
wapatanishi kutoka Jumuiya ya maendeleo ya serikali za kanda ya
Afrika Mashariki IGAD.
Hakuna upande uliotoa maelezo ya
kina kuhusu makubaliano hayo lakini wamesema watakutana tena Februari 20
kukamilisha maswala yote kwenye mkataba huo.
Wote, Kiir na Machar wametia saini
mikataba mingine hapo awali lakini ikavunjika. Mpatanishi wa IGAD Seyoum Mesfin
alionya kuwa yeyote atakayevunja makubaliano yaliyotiwa saini hivi
karibuni, ataripotiwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
No comments:
Post a Comment