Mwana wa gwiji wa muziki marehemu
Whitney Houston Bobbi Kristina jumamosi alipatikana akiwa kichwa chake
kiko ndani ya maji na asiye na fahamu katika beseni la kuogea lililokuwa
limejaa maji nyumbani kwake.
Walitafuta usaidizi wa 911 na kufanya matibabu ya dharura hadi maafisa wa usalama walipowasili na kujaribu kumfanya apumue.
Brown alipelekwa katika hospitali ya North Fulton ambapo anaendelea vyema na matibabu.
Hakuna anayejua kilichosababisha hali hiyo.
Maafisa wa matibabu wanasema kuwa wachunguzi hawajapata ushahidi wowote kubainisha kwamba kilikuwa kisa cha utumizi wa mihadarati ama pombe.
Polisi waliitembelea nyumba hiyo hivi majuzi baada ya mtu kuripoti kwamba kumekuwa na vita na baada ya kupolisi kugonga mlango bila mafanikio waliondoka.
No comments:
Post a Comment