Tangu siku kadhaa hakuna shambulio lolote limeshatokea katika mji wa Diffa. Hata hivyo raia wameendelea kuwa na hofu ya kutokea kwa mashambulizi ya aBoko Haram.
Takribani wakimbizi 4000 wamewasili tangu Jumatatu wiki hii katika mji wa Zinder, kwa mujibu wa viongozi wa mji huo. Hata kama hali ya usalama inajiri katika mji wa Zinder, raia wana wasiwasi ya kushambuliwa kutokana na kuwepo kwa wapiganaji wa Boko Haram katika malori wakiwasili katika mji wa Diffa.
“ Sote tunazungumzia suala hilo : mashambulizi, hususan kutegwa kwa mabomu, kwa kweli tunatiwa wasiwasi na hali hii. Tumetoa weto kwa watu wote kuwa makini na kudumisha mshikamano”, amesema El Hadj Ilia, mmoja kati ya mawakilishi wa mashirika ya kiraia.
Wanajeshi na askari polisi wameongezwa katika mitaa ya mji wa Zinder, huku baadhi yao wakionekana wakipiga doria kama msituni. Mkuu wa mji wa Zinder , Kalla Moutari, amebaini kwamba hatua za kuimarishwa kwa usalama zimepelekea watu kadhaa wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram wanakamatwa.
" Kuna uwezekano wanamgambo wa Boko Haram kujipenyeza katika raia wanaoukimbia mji wa Diffa, anasema. (...) Lakini kwa sehemu kubwa, maisha ni ya kawaida katika mji wa Zinder. Tumewataka raia kuwa makini. hiyo inamaanisha kuwa wanapoona kitu, wanapaswa kututaarifu. Miongoni mwa wakimbizi, tumewaondoa watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa boko Haram", amesema El Hadj Ilia.
Madereva wametakiwa kutoia taarifa mapema kwa wahusika iwapo wataona jambo lolote baya au linalotia wasiwasi kwa usalama wa raia.
No comments:
Post a Comment