Friday, 26 June 2015

ENYEMA na KOCHA WAWEKWA KITI MOTO ....!


Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) limewaweka kitimoto kipa wao mkongwe, Vincent Enyeama na kocha Stephen Keshi kwa madai ya utovu wa nidhamu na kukiuka kanuni za maadili walizosaini.

Enyeama, 32, anayeongoza kwa kuchezea zaidi timu ya taifa – Super Eagles, anashitakiwa kwa kusema hadharani kwamba hawakutakiwa kucheza jijini Kaduna dhidi ya Chad, akieleza kwamba usalama haungekuwapo.

Hiyo ilikuwa wakati wa mechi ya kwanza ya kutafuta kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2017. Keshi anatakiwa kujibu mashitaka ya kuomba kazi ya kuifundisha Timu ya Taifa ya Ivory Coast, muda mfupi tu baada ya kupewa kazi ya kudumu na NFF.

Enyeama anasema kwamba alidhani suala lake limemalizika kwa sababu alitakiwa aombe radhi na kufanya hivyo mara moja, lakini sasa NFF inahoji kwa nini hakufika kwenye kikao cha kusikiliza kesi yake wiki hii.

Kipa huyo anasema kwamba wala hajapata barua inayomwita kwenye kikao hicho. Keshi kwa upande wake anadai kwamba hajapata kuomba kazi Ivory Coast, bali wakala ambaye hata hivyo hakumtaja jina, ndiye alipeleka maombi hayo bila kumuarifu.

Ivory Coast wanatafuta kocha kwa ajili ya timu yao ya taifa – Tembo – na baada ya makocha au mawakala kutuma maombi, shirikisho la soka la huko lilibandika hadharani majina ya makocha 59 walioomba, wakiwamo Wafaransa na Waitaliano wengi, Mwingereza mmoja na Keshi.
Ivory Coast wanatafuta mrithi wa Herve Renard aliyewapa ubingwa wa Afrika na kisha kuondoka kwa ajili ya kufanya kazi nchini Ufaransa.

Ofisa wa ngazi za juu wa NFF, Chris Green amenukuliwa na vyombo vya habari vya Nigeria akisema kwamba watatuma ujumbe Abidjan, Ivory Coast kwa ajili ya kupata ukweli juu ya uombaji kazi wa Keshi kabla ya shauri lake kusikilizwa.

Kamati ya Utendaji ya NFF itatoa uamuzi baadaye juu ya mchezaji na kocha huyo, lakini bado haijasema ni lini itafanya hivyo. Mechi nyingine ya kufuzu kwa AFCON baina ya Nigeria na Misri imepangwa pia kufanyika jijini Kaduna.

Nigeria imekuwa ikiandamwa na mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa genge la Boko Haram katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo, na ni kwa sababu hiyo Enyeama alitaka mechi ifanyike eneo lenye usalama zaidi.

FISI ALA WATOTO .. BAHI ...!

 
Bwana FISI akiwa katika mawindo yake ya kawaida ...

Watoto wawili wenye umri wa kati ya miaka miwili na mitano wameuawa na fisi katika Kijiji cha Mnkola, Kata ya Ibihwa wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma katika matukio mawili tofauti. 
                              
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Teya Kata ya Ilindi wilayani hapa, Paul Mwaja alisema kuwa watoto hao wameuawa katika matukio mawili ndani ya kipindi cha wiki moja.

Mwaja alisema tukio la kwanza lilitokea juzi ambapo mtoto mmoja wa kiume mwenye aliuawa na fisi wakati akiwa na wenzie wawili wamelala. “Alikwenda fisi katika eneo hilo na kumvuta (mtoto mmoja) na kumtafuna hadi akamuua,”alisema Mwaja.

Alisema usiku wa kuamkia jana, fisi huyo alirudi tena katika kijiji hicho na kumnyang’anya mama mmoja mtoto wake mdogo mwenye umri wa miaka miwili.

Mwaja alisema fisi huyo alimla mtoto huyo na kumbakisha kichwa na utumbo tu, hali iliyozua taharuki katika kijiji hicho.

Hata hivyo, alisema baada ya tukio hilo wananchi waliamua kufanya msako na kumkamata fisi huyo na kumuua.

Baba mzazi wa mtoto aliyeuawa usiku wa kuamkia jana aliyejitambulisha kwa jina moja la Mchamingi, alisema hawana imani kama fisi huyo kama ni wa kawaida kwani katika tukio la kwanza kabla ya kuuawa, alikimbilia katika kijiji jirani cha Bahi Makulu na kupotelea kwenye nyumba za watu.

HAT-TRICK YA GUERRERO ‘PREDETOR’ IMEIPELEKA PERU NUSU FAINALI YA COPA AMERICA KIULAIIINI .. toka SHAFII DAUDA

Peru nusu fainali
 
Goli tatu ‘hat-trick’ ya Paolo Guerrero ‘Predetor’ dhidi ya Bolivia inaipeleka Peru kiulaini kwenye nusu fainali ya michuano ya Copa America 2015 inayozidi kushika kasi huko nchini Chille baada ya Peru kuibuka na ushindi murua wa goli 3-1 kwenye mchezo wa robo fainali uliopigwa usiku ‘mwingi’ wa Alhamisi kuamkia leo (Ijumaa).
 
Peru nusu fainali 1
 
Zilimchukua dakika 20 tu Guerrero ambae ni straika wa klabu ya Corinthians kupachika bao la kwanza na kuanza kuitafuta hat-trick yake kwenye michuano hiyo akiunganisha krosi safi kutoka kwa Romel Quinonez. Dakika tatu baadae mkali huyo alizama tena wavuni kupiga goli la pili kabla hajashindilia msumari wa mwiso dakika 16 kabla ya mchezo kumalizika. Mshambuliaji wa zamani wa Wigan Athletic Marcelo Moreno aliipatia Bolivia goli la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati na mchezo huo kumalizika kwa Peru kutinga fainali kwa ushindi wa goli 3-1.
 
Ushindi huo unaifanya Peru ikumbane na wenyeji Chile kwenye mchezo wa nusu fainali ya mashindano hayo ya Copa America kwenye dimba la Santiago siku ya Jumatatu Juni 29 mwaka huu kutafuta tiketi ya kufuzu kucheza hatua ya fainali.
 
Peru nusu
 
Imebaki michezo miwili ya robo fainali ili kukamilisha timu nne za kukipiga kwenye michezo miwili ya nusu fainali, Argentina itakipiga dhidi ya Colombia Jumamosi Juni 27 kwenye mchezo wa robo fainali wakati siku hiyo pia Brazil itakuwa ikimenyana na Paraguay kwenye mchezo mwingine wa robo fainali.

Thursday, 25 June 2015

MAKAMU WAKE WA RAIS KALAZA .. SPIKA WA BUNGE , .. KALAZA ! BADO NKURUNZINZA ANAKWAMBIA .. UCHAGUZI UPO PALE PALE .. dyu !

 
Gervais Rufyikiri aliyekuwa makamu wa rais wa Burundi amekimbilia Ubelgiji.

Serikali ya Burundi imesema haitashiriki katika mazungumzo yaliyodhaminiwa na Umoja wa Mataifa yakilenga kupunguza hali ya uhasama uliopo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wenye utata.
Waziri wa mambo ya ndani, Edouard Nduwimana, amsema ratiba ya uchaguzi haitabadilika.
Maandamano yamekuwa yakiendelea kwa wiki kadha kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kutaka kuwania nafasi ya urais kwa mara ya tatu.
Viongozi wawili katika serikali ya Rais Nkurunziza - akiwemo mmoja wa makamu wa rais, Gervais Rufyikiri, na spika wa bunge la nchi hiyo, Pie Ntavyohanyuma, wamekimbilia Ubelgiji.

Wote wawili wamekuwa wakosoaji wa rais. Uchaguzi umepangwa kufanyika mwezi uajao. Uchaguzi wa wabunge unafanyika Jumatatu.

SHUTUMA KWA POLISI WA SA .... WALIUA RAIA WAKUTOSHA !

 
polisi afrika ya KUSINI .
 
Tume ya uchunguzi nchini Afrika kusini imetaka ufanyike uchunguzi dhidi ya Polisi kuhusu mauaji ya wafanyakazi 34 wa mgodi yaliyofanyika mwaka 2012.
Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma amesema uchunguzi umebaini kuwa Polisi walikuwa na mpango usiofaa kumaliza mgomo katika mgodi mgodi wa Marikana na ilikuwa makosa kuutekeleza.

Wakati wote Polisi wamekuwa wakidai kuwa walikuwa wakijihami wakati wa mgomo wa wafanyakazi waliokuwa wakidai kuongezwa kwa mishahara.
Rais Zuma ameliita tukio hilo kuwa baya na kusema kuwa halina nafasi katika Demokrasia ya nchi hiyo.

Mauaji ya Marikana yanaelezwa kuwa mabaya kutokea nchini Afrika kusini tangu baada ya kumalizika kwa ubaguzi wa rangi miaka 20 iliyopita.

Wafanyakazi wa mgodi waligoma kwa siku kadhaa,na watu 10 tayari walipoteza maisha wakiwemo watu ambao hawakuwa kwenye mgomo, walinzi wa mgodi na Polisi, kabla ya tukio la tarehe 16 Agosti.

YA KI NEGA ' SUGU NA FAIZA ....

 ffffff
Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mheshimiwa Joseph Mbilinyi ‘Sugu akiwa na mwanaye. 
 
BAADA ya Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mheshimiwa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kuripotiwa kumfikisha mahakamani mzazi mwenziye, Faiza Ally, Juni 19, mwaka huu akitaka mahakama impe haki ya kumlea mtoto wao, Sasha (2), sakata limeisha kwa Sugu kukabidhiwa mtoto amlee.

faiza_ally666 
Mzazi mwenziye, na ‘Sugu’ Faiza Ally.

Katika hukumu ya kesi hiyo iliyosomwa juzi Jumanne huku upande wa mlalamikaji ambaye ni Mhe.  Sugu ukiwakilishwa na mwanasheria wake kutokana na Sugu kuwa bungeni mjini Dodoma, mdaiwa Faiza alionekana kubanwa na baadhi ya vielelezo huku suala la maadili likiwa ndiyo sababu kuu ya kumkosesha haki ya kumlea mtoto huyo.

HUKUMU ILIVYOTOLEWA

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi Patrick Vaginga wa Mahakama ya Mwanzo Manzese/Sina jijini Dar,  alisema baada ya kupitia maelezo ya pande zote mbili, yaani mlalamikaji ambaye ni Sugu na mlalamikiwa ambaye ni Faiza, mahakama hiyo imempa Sugu haki ya malezi ya mtoto kutokana na upungufu wa malezi ya mama ambaye ni Faiza.

FAIZA AKIRI

Hakimu Vaginga alisema kuwa kutokana na mlalamikiwa kukiri vielelezo vyote vya picha za nusu utupu ambavyo mlalamikaji, Sugu aliviwasilisha dhidi yake, mahakama imeona kumwacha mtoto kwa mama kutaathiri makuzi  kwa kuwa mtoto hujifunza haraka akiwa katika umri huo hasa kupitia mama.

VILIVYOMPONZA FAIZA

Hakimu huyo alivitaja baadhi ya vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo na Sugu kuwa ni picha ya Faiza akiwa amevaa pampasi.

Picha hiyo ilipigwa kwenye ‘bethidei’ yake, Desemba 18, mwaka jana. Picha akiwa amevaa shati tu ambayo alipigwa kwenye shoo ya Zari iliyojulikana kwa jina la Zari All White Party iliyofanyika Mei Mosi, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar.
Hakimu Vaginga aliitaja picha nyingine kuwa ni ile ya kigauni kifupi kilichoacha makalio nje. Alipigwa kwenye hafla ya Tuzo za Kili Music iliyofanyika Juni 13, mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City.

FAIZA AANGUA KILIO MBELE YA HAKIMU

Mara baada ya hukumu hiyo kusomwa, Faiza alishindwa kujizuia na kuangusha kilio mfululizo mbele ya hakimu, ikabidi atoke nje akisindikizwa na askari ili kuwezesha mahakama kuendelea na kesi nyingine.

FAIZA BAADA YA KUNYAMAZA KULIA

Baadaye akiwa ameacha kulia, waandishi wetu walimfuata Faiza akiwa ndani ya gari na kumuuliza alivyojisikia kufuatia hukumu hiyo, akasema:
“Siwezi kusema lolote lakini Mungu anajua. Mimi siwezi kuishi bila mwanangu Sasha. Nawaambia nitakufa. Sidhani kama wiki itapita mimi sijafa.”

LOADED ...

Here is how much 12 leading President and Prime Ministers get as their annual salaries. Not monthly o, annual! President Obama leads the pack with $400,000. South African President Jacob Zuma is the only African President in the list with an annual salary of $223, 500. Despite running the 2nd largest economy in the world, Chinese President is the 12th in the ranking with an annual salary of $22,000

.
                                 

AFRIKA YA KUSINI HUENDA IKAJITOA ICC ...

  

Afrika Kusini imesema kuwa huenda ikajiondoa kutoka kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC yenye makao yake makuu huko Hague Uholanzi kufuatia jaribio la kumkamata rais wa Sudan Omar al Bashir alipokuwa nchini humo majuzi.

Hata hivyo Nusra akamatwe kufuatia agizo la mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita dhidi yake kutokana na mashtaka ya mauaji ya kimbari.
Lakini baada ya kikao maalum cha baraza la mawaziri nchini humo, serikali ilitoa onyo kuwa huenda ikalazimika kujiondoa kutoka kwa makubaliano yeyote na mahakama ya ICC kutokana na sababu kadha.
 
null
Rais huyo wa Sudan alikuwa nchini Afrika Kusini kwa mkutano wa viongozi wa bara Afrika
''Serikali inawajibu wake wa kimataifa lakini pia inawajibu wake kisiasa''taarifa hiyo ilisema.
''iwapo hatutakuwa na suluhisho maalum itakayotusaidia kutanzua taharuki iliyopo kwa sasa nafikiri serikali yetu haitakuwa na budi ila kujiondoa kutokana na makubaliano yeyote na ICC''iliendelea kusema.

Mahakama ya Afrika Kusini ilikuwa imemuagiza rais Bashir kusalia nchini humo huku ikijadiliana kuhusu iwapo agizo hilo la kukamatwa kwake litekelezwe au la.

Lakini kabla ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wake rais Bashir aliondoka nchini Afrika Kusini na kurejea nyumbani.
 
null
Rais Bashir alipokewa kwa shangwe na nderemo aliporejea Khartoum
Rais huyo wa Sudan alikuwa nchini Afrika Kusini kwa mkutano wa viongozi wa bara Afrika na kwamba serikali ilikuwa inajua kwamba ilihitajika kumkamata kwa kuwa ni mwanachama wa ICC.

Kwenye taarifa yake , ICC ilisema kuwa waranti mbili za kumkamata Bashir bado zipo.

Rais al Bashir anatafutwa na mahakama ya uhalifu wa kivita kuhusiana na uhalifu ulitokea katika jimbo la Darfur na anakabiliwa na kesi inayohusiana na uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki.

K. . KUFIKISHWA MAHAKAMANI LEO ...

Kiongozi wa ujasusi wa Rwanda anatarajiwa kufika mahakamani hivi leo kuhusu madai ya uhalifu wa kivita yanayomkabili.
Luteni jenerali Karenzi Karake alizuiliwa katika uwanja wa ndege wa Heathrow Jumamosi chini ya kibali cha kukamatwa cha ulaya.
 
null
Waandamanaji wanaopinga kukamatwa kwa KK wako nje ya ubalozi wa Uingereza Kigali
Anatakiwa Madrid kuhusiana na vifo vya wafanyikazi wahispania waliokuwa wakihudumia mashirika ya misaada na mauji ya kimbari nchini Rwanda.
Rwanda imeonyesha masikitiko yake na kukamatwa kwake.
 
null
Waandamanaji wanaopinga kukamatwa kwa KK wako nje ya ubalozi wa Uingereza Kigali
Luteni jenerali Karenzi Karake, mwenye umri wa miaka 54 ni mtu wa kwanza wa ngazi ya juu kutoka kwa orodha ya watu 40 walio na wadhfa mkubwa katika jeshi la RPF orodha iliyotolewa na jaji mmoja wa Uhispania akitaka wakamatwe.
 
null
Waandamanaji wamepinga kuzuiliwa kwake
Wanakabiliwa na mashtaka ya madai ya kuhusika katika vitendo vinavotajwa kuwa uhalifu wa kivita uliofanyika dhidi ya wahutu mnamo mwaka 1990 huko Kazkazini mwa Rwanda.
Miongoni mwa wanaodaiwa kufariki kutokana na matukio hayo ni raia watatu wa Uhispania waliokuwa wakifanya kazi ya kutoa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo la kazkazini mwa Rwanda.
 
null
Luteni jenerali Karenzi Karake alizuiliwa katika uwanja wa ndege wa Heathrow jumamosi
Jaji muhispania Fernando Merelles ndiye aliyetoa warranti hizo na kutaka wakamatwe,agizo alilolitoa tangu February 2008 .
 
null
Karenzi Kareke kufikishwa mahakamani leo
Serikali ya Rwanda imeghadhabishwa na waranti hizo ikisema hazina msingi wowote.
Rwanda imekuwa ikishtumu hatua hiyo ya jaji Merelles na kusema ni kutumiwa vibaya na mahasimu wa serikali wenye misimamo mikali na kwamba
jaji huyo hajachukua hatua zipasavyo kupata mashahidi kutoka Rwanda au hata kufanya kazi pamoja na mahakama za Rwanda.

ONE DAY ' I WILL BE THE NEXT PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC .

                                                       

                     



obama 

                             10940618_1073063206053252_5133787841020524038_n  

                 obama2  

                  obama3  

In 1987 Barack Obama at the age of 26 visited his father’s homeland for the first time. He met his brothers, sisters and grandmother and later he said, the visit was to transform his life. The images below come from that trip to connect with his African roots. What a transformation from an unknown young African man to the leader of the free world.

Wednesday, 24 June 2015

VYUO 16' VIMESHUSHWA HADHI NA VYUO V 3' VIMEFUTWA KABISA NA NACTE

 

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam(hawapo pichani)wakati wa kutangaza ubora wa elimu ya ufundi inayotolewa na baraza hilo.Baraza hilo limevifuta usajili vyuo  vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.Kushoto ni Mkurugenzi wa Mitaala wa baraza hilo Twilumba Mponzi na Msaidizi wa katibu Mtendaji Alex Nkondola.

HOTUBA YA KAIMU KATIBU MTENDAJI WA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE) DKT ADOLF B. RUTAYUGA KUHUSU TAMKO LA BARAZA LA KUVIFUTIA USAJILI BAADHI YA VYUO NA KUVISHUSHA HADHI VINGINE - 24/06/2015

Ndugu waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, ninayo furaha kubwa kuwakaribisha katika ofisi za Baraza. Lengo la kuwaita hapa leo ni kuwapa taarifa juu ya maamuzi yaliyofikiwa na Baraza ikiwa ni katika jitihada za kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini.

Ndugu Waandishi wa Habari

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, kwa lengo la kusimamia na kuratibu taaluma zinazotolewa na taasisi na vyuo vva elimu ya ufundi nchini, ambavyo siyo vyuo vikuu au vyuo vikuu vishiriki. Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini kwa kusimamia kikamilifu shughuli za kuendesha mafunzo ili tuzo zinazotolewa na taasisi na vyuo ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa.

 Kwa kutumia Sheria na Kanuni za Baraza za Usajili (2001) na zile za Ithibati na Utambuzi (2001), mnamo tarehe 20 Februari 2015, Baraza lilitoa notisi ya siku 30 kwa taasisi na vyuo vilivyokiuka taratibu na vyenye mapungufu makubwa ya Usajili na Ithibati kupitia taarifa yake kwa Umma. Notisi hii ililenga kuzipa taasisi na vyuo nafasi ya kujirekebisha. 

 Baraza linakiri kuwa taasisi na vyuo vingi kama vilivyoorodheshwa kwenye Jedwali Na. 1, Jedwali Na. 3, na baadhi kwenye Jedwali Na. 5 vimechukua hatua mbalimbali za kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza. Hata hivyo, hadi kufikia leo tarehe 24 Juni 2015 yaani siku 124 baada ya Notisi ya Baraza, kuna vyuo ambavyo havijachukua hatua yoyote ya kurekebisha mapungufu yake kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 2 na Jedwali Na. 4.

 Tamko la Baraza

 Kutokana na mapungufu hayo Baraza limeamua kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zake kwa taasisi na vyuo vyote vilivyoorodheshwa katika Jedwali Na. 2 na Jedwali Na. 4 kwa makosa yafuatayo:

a)    Ama kumalizika kwa muda wa  Usajili wa Awali (Preparatory Registration) na Usajili wa Muda (Provisional Registration); au
b)    Kutoanza mchakato wa kupata Ithibati baada ya kupata Usajili Kamili; au
c)    Kumalizika kwa muda wa Ithibati na kutochukua hatua ya kuomba upya Ithibati (re-affirmation); na
d)    Taasisi na Vyuo kuamua vyenyewe kusitisha kutoa mafunzo kwa sababu mbalimbali.

ok...!

WAANDIKISHAJI WAFUNGIWA VYUMBANI HUKO GEITA ... dyu !

 

Kazi ya uandikishaji wapigakura imezidi kukumbwa na matatizo baada ya wananchi kuwafgungia waandikishaji ndani ya kituo kutokana na kupata taarifa kuwa muda uliopangwa kwa ajili ya mitaa ya Buhalahala, Kisesa na Moringe umekwisha, huku wakiwa hawajapata nafasi ya kusajiliwa.
 
Wakati vurugu hizo zikitokea, wananchi wa kata nne za wilayani Bukombe wanahofia kukosa nafasi ya kuandikishwa kutokana na maeneo yao kutoingizwa kwenye mfumo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), huku watu watatu, wakiwamo watoto wawili wilayani Hanang wakikamatwa kutokana na kujiandikisha mara mbili huku wakiwa hawajafikia umri unaotakiwa.
Tukio la Geita limetokea siku chache baada ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuwataka wananchi mkoani Kilimanjaro kutoruhusu mashine zinazotumika kuandikishia wapigakura kwa njia ya kielektroniki (BVR) kuondolewa vituoni endapo kuna watu ambao hawajaandikishwa.
Uandikishaji mkoani Geita ulianza Juni 17, mwaka huu kwa kata tatu za Buhalahala, Mwatulole na Kalangalala na muda uliopangwa kumalizika ni juzi. Hali ilikuwa mbaya kwenye kata hizo baada ya wananchi kukaa vituoni hadi usiku wakisubiri kuandikishwa, na walipopata taarifa kuwa kazi hiyo haitaendelea kwa kuwa siku zilizopangwa zimemalizika, walichukua uamuzi huo wa kuzuia waandikishaji hadi watakapoandikisha wote waliokuwa wamesalia.
“Nimekuja hapa nina siku ya tano leo (juzi). Kila nikija sipati nafasi ya kuandikishwa wengine wanakesha vituoni siku ya tano, lakini hawajaandikishwa na leo ndiyo mwisho,” alilalamika mkazi wa Mwatulole, Marwa Ernest.
Mkazi mwingine, Neema Charles alisema:“Mwandikishaji anatuambia macho hayaoni, kwa hiyo sisi tufanyeje, tunataka kitambulisho kwani ndiyo cha msingi mwaka huu.”
Wananchi hao ambao walionekana kuwa na jazba, huku wakitishia kuchoma mashine kama wasingeandikishwa, walidai kuwa shughuli hiyo imetawaliwa na rushwa.
Hali hiyo ilikikumba kituo cha Shule ya Sekondari ya Kalangalala, ambako hadi saa 1:30 usiku mwandishi alishuhudia zaidi ya wananchi 200 wakiwa kituoni wengine wakipigana na kusukumana kila mmoja akitaka kuandikishwa.
“Hapa muda unaisha na leo (juzi) ndiyo mwisho, hatujui hatima yetu, wananchi wengi hatujaandikishwa, tumeshaomba tuongezewe mashine lakini hatusikilizwi zaidi tunashuhudia wenye fedha ndiyo 
wanaandikishwa,” alisema mkazi wa Kisesa, Mariana Peter.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Hellen Kahindi alikiri kuwapo kwa vurugu hizo na kwamba walikosea kuweka vituo pembezoni mwa mji, jambo lililosababisha wananchi wa mjini kukimbilia maeneo hayo wakihofia kutoandikishwa.
Alisema vurugu hizo zilisababisha magari mawili ya Serikali kuvunjwa vioo, huku waandikishaji wakiponea chupuchupu kutokana na kuwapo na vurugu kubwa eneo la kutokea hadi polisi walipoingilia kati.
“Tunashukuru hakuna madhara makubwa yaliyotokea kwa waandikishaji na vifaa, lakini tumejipanga kwa zoezi hili jipya ili matatizo hayo yasijitokeze kwani tumeongeza wino na kwenye mashine,” alisema Kahindi.

Wakati huohuo; wananchi wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, huenda wakashindwa kuandikishwa kutokana na kata zao nne kutowekwa kwenye mfumo wa utawala na hivyo kutotambulika na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Wakizungumza kwa nyakati tofauti juzi, maofisa wa kata hizo mpya za Katente, Katome, Bulangwa na Bulenga walisema maeneo yao hayamo kwenye mfumo wa NEC.
Ofisa mtendaji Kata ya Katome, Lukuba Shitwala alisema kutokana na kata yake kutokuwa kwenye mfumo huo, huenda zaidi ya wananchi 9,000 wakakosa kuandikishwa.
Hata hivyo, mkurungenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe, James Ihunyo alisema tayari kata hizo zimeingizwa NEC, licha ya awali kutokuwamo, hivyo akawaomba watendaji kuhamasisha wananchi kujitokeza vituoni.
Watoto wajiandikisha Hanang’
Watoto wawili wenye umri wa miaka 15 wa Kijiji cha Nangwa, wilayani Hanang’ na mtu mwingine mmoja wilayani Babati mkoani Manyara wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kujiandikisha zaidi ya mara tatu huku wakiwa hawajafikia umri wa 18 unaotakiwa.
Mkuu wa mkoa wa Manyara, Joel Bendera alisema atahakikisha wote wanafikishwa mahakamani ili wachukuliwe hatua kali za kisheria kwa kuwa alishapiga marufuku watu kujiandikisha zaidi ya mara moja.
Mbali na watoto hao, mtu mwingine alijiandikisha mara tatu ni mkazi wa Boay wilayani Babati aliyetumia majina tofauti, akiitwa Petro Hhari kwenye kituo cha Shule ya Msingi ya Ditsoma A, Peter Tluway katika kituo cha zahanati na Peter Hary katika kituo cha ofisi ya kijiji hicho.
Mratibu wa BVR mkoani Manyara, Mwajabu Nyamkomola alithibitisha kupata taarifa za matukio hayo.
Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Mahamud Kambola alisema uandikishwaji unaendelea vizuri na wananchi wajitokeze.

KOBE WANATOROSHWA' WAKAMATWA AIPORT JNIA




 
KOBE

Jeshi la Polisi, Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNAI), linamshikilia, raia wa Kuwait, Hussein Mansoor, kwa kukutwa na kobe hai 173 aliokuwa akiwasafirisha kueleka nchini kwake.

Kaimu Mkurugenzi wa Uwanja wa JNIA, Clemence Jingu alisema abiria huyo mwenye hati ya kusafiria yenye namba 003870237, alikamatwa usiku wa kuamkia jana akijitayarisha kupanda ndege ya Emirates iliyokuwa ikielekea Kuwait kupitia Dubai.
Jingu alisema raia huyo alikamatwa saa tano usiku katika eneo la abiria wanaoondoka, baada ya polisi wa JNIA kwa kushirikiana na maofisa wa Wizara ya Maliasili kufanya ukaguzi na kugundua kobe hao wakiwa wamefichwa kwenye masanduku makubwa mawili.
“Hii ni moja ya kazi kubwa ambazo tunazifanya kwa sasa hapa JNIA, ila tutahakikisha kuwa hakuna nyara za Serikali zitakazotaifishwa na kupitishwa hapa kwa kuwa tumeimarisha ulinzi maradufu,” alisema Jingu.
Jingu alisema kobe hao wenye thamani ya Sh 30 milioni ni miongoni mwa nyara muhimu za Serikali ambazo zimekuwa zikitaifishwa kupitia mbinu mbalimbali.
“Pamoja na kuimarisha ulinzi, lakini tutahakikisha JNIA inakuwa bora kuliko viwanja vingine vya Afrika Mashariki na zaidi hasa kuhakikisha ulinzi unapewa kipaumbele” alisema.
Kamanda wa Polisi wa JNIA, Khamis Suleiman, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi.
Tukio hilo lilithibitishwa pia na Kamishna wa Interpol, Tawi la Tanzania, Gustav Babile ambaye alisema raia huyo alikamatwa na wanyama hao huku akiwa na vibali halali.
Mmoja wa wafanyakazi wa JNIA (jina linahifadhiwa) alisema kabla ya kukamatwa, ilionekana kuna mpango umefanywa ili kumpitisha raia huyo bila kugundulika kwani taa za eneo la ukaguzi zilizimwa kwa saa kadhaa uwanjani hapo.
“Si kawaida taa kuzimwa lakini wakati yeye anapita taa zilizima jambo linaloonyesha kuwa ni njama zilizopangwa lakini hata hivyo hazikufanikiwa,” kilisema chanzo hicho.
Kadhalika chanzo hicho kilisema raia huyo aligunduliwa na askari wa maliasili akiwa tayari ameshapita katika vizuizi vyote vya ukaguzi na ameshaingia katika eneo la abiria wanaoondoka.
Tukio hili linafanana kwa kiasi kikubwa na lile lililotokea Januari 8, mwaka huu, ambapo raia mwingine wa Kuwait, Ahmed Ally Mansour alikamatwa uwanja wa JNIA akiwatorosha kenge hai 149 wenye thamani ya Sh 6.3 milioni.

Kama ilivyo kwa tukio la jana, hata tukio la Januari lilitokea saa tano, likihusisha ndege ile ile huku watuhumiwa wakiwa na ubini unaolandana.
Kadhalika, Julai 31 mwaka jana, raia wa Vietnam, Dong Van (47) naye alikamatwa uwanjani hapo akiwa na meno 65 na kucha 447 za simba zenye thamani ya Sh189.4 milion

HATUTAVUMILIA TISHO LA USALAMA ... UFARANSA ''

 
 Francois Hollande

Serikali ya Ufaransa sasa imemtaka balozi wa Marekani nchini humo kufika mbele yake kufuatia madai kwamba Marekani iliwachunguza watangulizi wake wawili.

Mtandao wa Wikileaks unasema kuwa kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA kilimpeleleza rais Hollande,Nicholas Sarkozy na Jacques Chiraq kati ya mwaka 2006-12.

 
null
Marais wa Ufaransa
Bwana Hollande ameitisha kikao cha dharura na kusema Ufaransa haitavumilia vitendo ambavyo ni tishio kwa usalama wake.
Hatahivyo Marekani imesema kuwa haitatoa tamko kuhusu madai fulani ya kiintelijensia.

Ned Price ambaye ndio msemaji wa Baraza la kitaifa la usalama nchini Marekani ameongozea kwamba Marekani hailengi na wala haitalenga mawasiliano ya Hollande.
 
null
Wikilieaks
Shirika la NSA lilishtumiwa kwa kumpeleleza kansela wa Ujerumani Angela Merkel pamoja na viongozi wa Brazil na wale wa Mexico.

SERA JUU YA MATEKA KUBADILISHWA MAREKANI ...!

 
 RAIS WA MAREKANI : BARACK H. OBAMA

Rais wa Marekani Barack Obama ametoa tamko la kubadilishwa kwa sera za nchi yake katika masuala ya kubadilishana ama kuwakomboa mateka ambao ni raia wake.

Rais ametiulia mkazo kauli yake, amesema kwamba seriakali yake haitafanya makubaliano yoyote yenye lengo la kuwakomboa mateka ambao ni raia wa Marekani waliotekwa ughaibuni,lakini aliweka bayana juu ya familia ambazo huamua kulipa fidia ya ndugu zao mateka kwamba hawatakabiliwa na mashtaka.

Rais Obama ameeleza kuwa anatambua wazi kuwa familia za mateka huwa wanachaganyikiwa pindi wanapo shughulika na serikali yao wenyewe.

Ameelezea pia mipango ya baadaye ya serikali yake na sera za nchi hiyo kwamba
kutakuwa na utaratibu maalum kiserikali kuratibu jitihada za vitengo mbali mbali na taasisi zingine zinazojitahidi kuwaokoa mateka ambao ni raia wa Marekani .Ahadi ya Rais Obama kwa raia wake ni kuchukua hatua stahiki kuwarejesha raia wake nyumbani na kuwachukulia hatua watekaji wao.

Ujumbe wangu kwa kila raia wa Marekani ambaye anashikiliwa mateka popote ulimwenguni,ni huu Marekani haitaacha kuhakikisha unaungana na familia yako.hatutasita,hata kama itatuchukua muda mrefu kiasi gani.

MWAKA 1987 NILIKUA NA MIAKA MIWILI KASORO HIVI .. BARACK OBAMA ALITEMBELEA KIJIJI CHA BIBI YAKE KWA MARA YA KWANZA NCHINI KENYA

obama 

                             10940618_1073063206053252_5133787841020524038_n  

                 obama2  

                  obama3  

In 1987 Barack Obama at the age of 26 visited his father’s homeland for the first time. He met his brothers, sisters and grandmother and later he said, the visit was to transform his life. The images below come from that trip to connect with his African roots. What a transformation from an unknown young African man to the leader of the free world.

CHILE YATINGA NUSU FAINALI COPA AMERICA, URUGUAY YAZODOLEWA KADI MBILI NYEKUNDU toka shafii dauda

29F26CA600000578-3138343-image-a-54_1435195099638
Timu ya Taifa ya Chile imetinga nusu fainali ya michuano ya mataifa ya America kusini (Copa America) baada ya kuitandika Uruguay  goli 1-0 katika mechi ya robo fainali iliyopigwa usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Santiago.
Goli pekee la wenyeji Chile lilifungwa na Mauricio Isla katika dakika ya 81′.
Isla slams in the winner to settle the tie as Uruguay's despairing defenders try to dive in to stop him scoring - in vain
Dakika ya 63′ Uruguay ilipata pigo baada ya mshambuliaji wake Edinson Cavani kuoneshwa kadi nyekundu kufuatia kuoneshwa kadi ya kwanza ya njano kwa kosa la kumtukana mwamuzi wa mechi.
Wakati huo huo  beki Jorge Fucile naye alioneshwa kadi ya pili ya njano na hatimaye nyekundu katika dakika ya 90′ baada ya kumchezea vibaya Alexis Sanchez wa Chile.
Kwa matokeo hayo, Chile itacheza nusu fainali dhidi ya mshindi wa mechi ya robo fainali itakayowakutanisha Bolivia na Peru.

PAPA MUSOFE HURUUU ...!




Papaa Msofe akiwa mahakamani. (Picha kutoka maktaba yetu)

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imemfutia kesi ya mauji iliyokuwa ikimkabili mfanyabishara maarufu nchini, Marijan Abubakar, maarufu kama 'Papaa Msofe' baada ya kupokea taarifa kutoka kwa MKurugenzi wa Mashitaka (DPP), Biswalo Mganga leo kuwa hana nia ya kuendelea kumshitaki tena.



 Kwa mujibu wa Kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, inampa mamlaka DPP kuifuata kesi ya jinai bila kuhojiwa na mtu yeyote wala mamlaka yoyote ile.

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA BURUNDI AHOFIA USALAMA ...

  Makamu wa pili wa rais wa Burundi, Gervais Rufyikiri, ambaye ametangaza kujiuzulu kwenye wadhifa wake.

Makamu wa pili wa rais nchini Burundi, Gervais Ruyikiri ametangaza kuwa hatorurudi nchini kama usalama wake utakua haujalindwa ipasavyo. 

Akizungumza kwenye televisheni ya Ufaransa France 24, Gervais Rufyikiri, amesema ameamua kufanya hivyo akihofia usalama wake kutokana na jinsi hali invyoendelea nchini Burundi.

Gervais Rufyikiri, ambaye ni mmoja wa vigogo wa chama tawala cha Cndd-Fdd amesema amemuandikia barua rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, akimuomba kuachana na mpango wake wa kuwania muhula wa tatu, akibaini kwamba ni kinyume na Katiba ya nchi pamoja na Mkataba wa amani na maridhiano wa Arusha.

Gervais Rufyikiri amesema rais Nkurunziza amekua hasikii hata nasaha anazopewa na taasisi za kimataifa pamoja na washirika wake wa karibu.
Wakati huo huo Spika wa Bunge la Burundi, Pie Ntavyohanyuma ameondoka nchini humo Jumatano Juni 24, akielekea nchini Ubelgiji. 

Haijafahamika iwapo kiongozi huyo wa taasisi muhimu nchini ameitoroka nchi hiyo au la. Lakini habari ambazo zimeendelea kusambaa mjini Bujumbura zinabaini kwamba Pie Ntavyohanyuma ameitoroka nchi.

Hayo yakijiri serikali ya Bujumbura ikiwakilishwa na waziri wake wa mambo ya ndani, Edouard Nduwimana, imeshiriki katika mazungumzo yanayolenga kutafutia ufumbuzi mgogoro unaoendelea kushuhudiwa nchini Burundi.

Mazungumzo hayo yameingia Jumatano wiki hii katika siku yake ya pili, baada ya kuanza Jumaanne Juni 23.

Katika siku yake ya kwanza, mazungumzo hayo yaliitikiwa na upinzani, mashirika ya kiraia pamoja na viongozi na wawakilishi wa dini mbalimbali.
Serikali ya Bujumbura na chama tawala pamoja na baadhi ya washirika wake walisusia mazungumzo hayo, wakibaini kwamba hawatashiriki mazungumzo hayo ambayo yanakuja kuwapotezea muda wakati ambapo wako katika siku za mwisho za kampenzi za uchaguzi wa wabunge na madiwani.

Jumatatu wiki hii timu ya usuluhishi iliwatolea wito wadau wote katika mgogoro wa Burundi kushiriki mazungumzo kwa minajili ya kutafutia suluhu mgogoro huo. Lakini Chama tawala cha Cndd-Fdd na serikali vimesusia kikao cha kwanza cha mazungumzo hayo.

Jumanne Juni 23 chama hicho cha rais Pierre Nkurunziza kilitangaza kuwa hakitashiriki kutokana na kampeni ya uchaguzi wa wabunge na madiwani ambayo kinaendesha wakati huu zikisalia siku zisiozidi sita ili ufanyike uchaguzi wa wabunge na madiwani.

Chama cha Uprona kinachotambuliwa na utawala wa Pierre Nkurunziza hakikushiriki mazungumzo hayo.

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa chama cha Uprona, Gaston Sindimwo, huu siwakati wa mazungumzo. " Mazungumzo yanakaribishwa baada ya uchaguzi, hapana wakati huu", amesema gaston Sindimwo.

Itafahamika kwamba chama cha Cndd-Fdd kimekua kikifutilia mbali uwezekano wowote wa kuandaa kwa makubaliano ya wadau wote katika mchakato wa uchaguzi kalenda ya uchaguzi, pamoja na kuanzisha mazungumzo yatakayowashirikisha wadau wote.

Timu ya usulihishi wa kimataifa ilikutana Jumatatu wiki hii kwa mara ya kwanza mjini Bujumbura. Timu hii inaundwa na Ibrahima Fall kutoka Umoja wa Afrika, Abdoulaye Bathily kutoka Umoja wa Mataifa, Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Richard Sezibera pamoja na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR ).

Hayo yakijiri hali ya usalama imeendelea kudorora katika maeneo mbalimbali nchini Burundi, hususan katika mji mkuu wa Bujumbura.
Hali ya hofu imeendelea kutanda katika mji wa Bujumbura, huku kila upande ukiutuhumu mwengine kuhusika na mdororo wa usalama unaoshuhudiwa wakati huu nchini Burundi.