Waziri mkuu wa Australia Tony Abbot
hajapinga ripoti kuwa maafisa wake mpakani mwa taifa hilo waliwalipa
walanguzi wa watu fedha ili kuirejesha mashua iliyokuwa imejaa wahamiaji
hadi Indonesia.
Bwana Abbot amesema kuwa, mikakati ya ubunifu inatumika ili kuzima mashua ya wahamiaji kuingia nchini humo.
Mwaandishi habari wa BBC mjini Sydney, anasema kuwa Australia imechukua uamuzi mgumu dhidi ya wahamiaji huku ikifanya kila mbinu kuzizuia mashua zinazowabeba wahamiaji kufika kwenye fukwe zake.
No comments:
Post a Comment