Monday, 15 June 2015

TAIFA STARS MAJANGA MATUPU ....!


 

Taifa Stars imeanza vibaya mechi za Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 baada ya kufungwa mabao 3-0 na Misri usiku huu mjini Alexandria. Mabao yote ya Misri yalipatikana kipindi cha pili, wafungaji Rami Rabia dakika ya 61, Basem Morsi dakika ya 65 na Mohamed Salah dakika ya 70. Huo unakuwa mchezo wa nne mfululizo Stars inafungwa chini ya kocha wake, Mholanzi Mart Nooij baada ya awali kufungwa mechi zote tatu za Kundi B Kombe la COSAFA mwezi uliopita 1-0 na Swaziland, 2-0 na Madagascar na 1-0 na Lesotho mjini Rusternburg Afrika Kusini. Kikosi cha Taifa Stars kilichifungwa 3-0 na Misri Mwinyi Kazimoto wa Taifa Stars (nyuma) akimfuatilia mchezaji wa Misri Kwa ujumla huo unakuwa mchezo wa 17 kwa Nooij tangu aanze kuinoa Taifa Stars Aprili mwaka jana akirithi mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen kati ya hizo akiwa ameshinda mechi tatu tu. Matokeo hayo yanaifanya Misri ianzie kileleni mwa Kundi G nyuma ya Nigeria ambayo jana iliifunga Chad mabao 2-0, wakati Stars inashika mkia. 

Tanzania watakuwa wenyeji wa Nigeria Septemba mwaka huu, wakati Misri watasafiri kuifuata Chad Kikosi cha Taifa Stars kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Aggrey Morris/Salim Mbonde, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Erasto Nyoni, Mwinyi Kazimoto/Simon Msuva, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, Amri Kiemba/Frank Domayo na Jonas Mkude. Misri: Ahmed El Shenawy, Ahmed Hegazy, Ramy Rabea, Mohamed Abd Elshafy, Hazem Emam, Mohamed Elneny, Ibrahim Salah, Mahmoud Abd Elmonem/Ramadan Soffiy, Mohamed Salah/Mostafa Ftahy, Doly Elgabay/Basem Morsy, Ahmed Hassan Meky. Katika michezo mingine ya leo, Ghana imeiadhibu Mauritius mabao 7-1 katika mchezo wa Kundi H kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika jioni ya leo Uwanja wa Ohene Djan Sports mjini Accrah. Mabao ya Ghana yamefungwa na Christian Atsu dakika ya 10, Jordan Ayew mawili dakika ya 17 na 38, Asamoah Gyan mawili pia dakika ya 23 na 30, Schlupp dakika ya 66 na Accam dakika ya 90, wakati bao pekee la Mauritius limefungwa na Jean-Pierre Sophie. Kocha wa zamani wa Yanga SC, Mbelgiji Tom Saintfiet ameanza vizuri kibarua chake baada ya kuiongoza kushinda 2-1 dhidi ya Liberia Uwanja wa Kegue mjini Lome. Equatorial Guinea imelazimishwa sare ya 1-1na Benin Uwanja wa Bata, Niger imeifunga 1-0 Namibia Uwanja wa Stade General S.K, Kongo imelazimishwa sare ya 1-1 na Kenya Uwanja wa Alphonse Massamba-Débat.

 Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij ameshinda mechi tatu tu kati ya 17 ambazo ameiongoza Taifa Stars hadi sasa Kenya walianza kupata bao kupitia kwa Paul Were dakika ya 10 kabla ya Prince Oniangue kuwasawazishia wenyeji kwa penalti dakika ya 36. DRC imepata ushindi mwembamba wa mabao 2- 1 dhidi ya Madagascar Uwanja wa Tata Raphael mjini Kinshasa, wakati Cameroon imeshinda 1-0 dhidi ya Mauritania mjini Yaounde, Ethiopia imeilaza 2-1 Lesotho Uwanja wa Addis Ababa, Rwanda imeshinda 1-0 ugenini dhidi ya Msumbiji Uwanja wa Zimpeto, Algeria imeichapa 4-0 Shelisheli Uwanja wa Mustapha Tchaker.

No comments:

Post a Comment