Maofisa wa afya nchini Sierra Leone
wamesema kwamba kuna wagonjwa wawili wapya wanaougua ugonjwa wa ebola na
kwamba wamegunduliwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Freetown.
Naye msemaji wa kituo cha karantini cha taifa hilo amesema kwamba kulikuwa na wasiwasi mkubwa kwasababu vituo vyote vya karantini na vitendea kazi vyake vilikuwa vimefungwa mjini Freetown.
Na akaongeza kusema kwamba kuna shaka kuwa kutatokea maambukizi mapya kutoka katika eneo lenye msongamano wa makazi duni.
Nako upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo ya Sierra Leone unaendelea kupata maambukizi mapya ya ugonjwa.
No comments:
Post a Comment