Polisi katika jimbo la South
Carolina nchini Marekani wamesema kuwa mtu mmoja aliyejihami kwa bunduki
amewapiga risasi na kuwaua watu tisa ndani ya kanisa la kimethodist.
Shambulio hilo limefanyika ndani ya kanisa la Emmanuel African Methodist Church, kanisa linaloaminiwa kuwa la zamani zaidi la kiafrika nchini Marekani
Polisi wamesema kuwa shambulio hili ni la chuki ya rangi ya ngozi.
No comments:
Post a Comment