Timu ya Taifa ya Chile imetinga
nusu fainali ya michuano ya mataifa ya America kusini (Copa America)
baada ya kuitandika Uruguay goli 1-0 katika mechi ya robo fainali
iliyopigwa usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Santiago.
Goli pekee la wenyeji Chile lilifungwa na Mauricio Isla katika dakika ya 81′.
Dakika ya 63′ Uruguay ilipata
pigo baada ya mshambuliaji wake Edinson Cavani kuoneshwa kadi nyekundu
kufuatia kuoneshwa kadi ya kwanza ya njano kwa kosa la kumtukana mwamuzi
wa mechi.
Wakati huo huo beki Jorge
Fucile naye alioneshwa kadi ya pili ya njano na hatimaye nyekundu katika
dakika ya 90′ baada ya kumchezea vibaya Alexis Sanchez wa Chile.
Kwa matokeo hayo, Chile itacheza nusu fainali dhidi ya mshindi wa mechi ya robo fainali itakayowakutanisha Bolivia na Peru.
No comments:
Post a Comment