Kiongozi wa ujasusi wa Rwanda anatarajiwa kufika mahakamani hivi leo kuhusu madai ya uhalifu wa kivita yanayomkabili.
Luteni jenerali Karenzi Karake alizuiliwa katika uwanja wa ndege wa Heathrow Jumamosi chini ya kibali cha kukamatwa cha ulaya.Anatakiwa Madrid kuhusiana na vifo vya wafanyikazi wahispania waliokuwa wakihudumia mashirika ya misaada na mauji ya kimbari nchini Rwanda.
Rwanda imeonyesha masikitiko yake na kukamatwa kwake.
Luteni jenerali Karenzi Karake, mwenye umri wa miaka 54 ni mtu wa kwanza wa ngazi ya juu kutoka kwa orodha ya watu 40 walio na wadhfa mkubwa katika jeshi la RPF orodha iliyotolewa na jaji mmoja wa Uhispania akitaka wakamatwe.
Wanakabiliwa na mashtaka ya madai ya kuhusika katika vitendo vinavotajwa kuwa uhalifu wa kivita uliofanyika dhidi ya wahutu mnamo mwaka 1990 huko Kazkazini mwa Rwanda.
Miongoni mwa wanaodaiwa kufariki kutokana na matukio hayo ni raia watatu wa Uhispania waliokuwa wakifanya kazi ya kutoa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo la kazkazini mwa Rwanda.
Jaji muhispania Fernando Merelles ndiye aliyetoa warranti hizo na kutaka wakamatwe,agizo alilolitoa tangu February 2008 .
Serikali ya Rwanda imeghadhabishwa na waranti hizo ikisema hazina msingi wowote.
Rwanda imekuwa ikishtumu hatua hiyo ya jaji Merelles na kusema ni kutumiwa vibaya na mahasimu wa serikali wenye misimamo mikali na kwamba
jaji huyo hajachukua hatua zipasavyo kupata mashahidi kutoka Rwanda au hata kufanya kazi pamoja na mahakama za Rwanda.
No comments:
Post a Comment