Monday, 15 June 2015

MASHAMBULIZI YA ANGA YAMUUA KIONGOZI MKUU WA ALQAEDA ....

 Kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la Al Qaeda, Mokhtar Belmokhtar aliyeuawa.

Kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la Al Qaeda, Mokhtar Belmokhtar ameuawa katika mashambulizi ya yaliyofanywa na Jeshi la Marekani nchini Libya.

Inasemekana kuwa, watu wengine kadhaa wameuawa wakati wa mashambulizi hayo.
Kwa upande wake, Wizara ya Ulinzi ya Marekani kupitia Makao Makuu ya Jeshi la nchi hiyo (Pentagon) imedai kuhusika na mashambulizi hayo wakikusudiwa kumlenga gaidi huyo (Mokhtar Belmokhtar) wa mtandao wa Al Qaeda.

Kanali Steve Warren, msemaji wa Pentagon amesema kuwa, mashambulizi hayo yalifanywa Jumamosi usiku na kwamba hivi sasa wanatathmini matokeo ya oparesheni yao hiyo.

Blmokhtar anaaminika kuwa ndiye aliyeongoza shambulizi kubwa la kigaidi katika kiwanda cha gesi nchini Algeria mwaka 2013, shambulzi lililosababisha vifo vya watu 35 wakiwemo raia watatu wa Marekani.  

No comments:

Post a Comment