
Wakazi wa kitongoji duni cha Mathare katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, sasa wanaweza kupata maji safi ya kunywa na kwa matumizi mengine.
Mpango unaoungwa mkono na serikali umezinduliwa kwenye mji mkuu wa Kenya Nairobi unaowawezesha watu wanaoishi kwenye mitaa ya mabanda kununua maji kwa kutumia kadi.Vituo vya kuuza maji vimebuniwa kote katika sehemu za mabanda ambapo wenyeji hutumia kadi zilizo na pesa kununua maji safi na kwa bei nafuu.

Mradi kama huo umefaulu katika baadhi ya maeneo ya vijijini nchini Kenya, lakini hii ni mara ya kwanza kuzinduliwa katika mji huo mkuu.

Kampuni ya kusimamia huduma ya usambazaji maji, ina mikakati ya kuhakikisha kuwa huduma hii walioianzisha itasambazwa kote katika mji mkuu wa Nairobi na kwengineko nchini humo.

Hongera kwa kenya kwa hatua walopiga hapa Tanzania hata hayo maji safi bado tatizo wangekuwa na amani kama huku wangefka mbali zaidi
ReplyDelete