Thursday, 11 June 2015

WALIMU 100 WAPIGWA CHINI KENYA .... >

Tume ya huduma ya walimu nchini Kenya, imewafungia zaidi ya walimu mia moja ambao kamati hiyo inasema imekuwa ikiwachunguza kwa makosa mbalimbali ikiwemo udhalilishaji wa kijinsia. Walimu hao kwa sasa wameondolewa usajili rasmi wa walimu na hawatoruhusiwa kurejea kufundisha nchini humo. Taarifa ya Robert Kiptoo inasomwa na Ally Bakari.

Taarifa iliyopatikana kwenye gazeti la serikali ya Kenya, Tume ya huduma ya walimu imetoa majina ya walimu 126 ambao wamesimamishwa kazi kwa madai ya tabia chafu.

Taarifa inasema kuwa walimu hao walifukuzwa kazi baada kupitia mchakato wa kinidhamu ambao umewakuta na hatia ya makosa mbalimbali.

Walimu wawili waliofutwa kazi ni wanawake.Taarifa hiyo ilionya kwamba, kama mwalimu yeyote kati ya waliofungiwa atadharau uamuzi huo, basi atapigwa faini ya hadi kufikia dola za Kimarekani 50 au kifungo kisichozidi miezi sita au vyote viwili.

                                      
                                 Mwenyekiti wa muungano wa wazazi nchini Kenya Musau Ndunda .

Miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko la idadi ya walimu ambao wamekuwa wakituhumiwa kwa tabia chafu huku baadhi nyao wakihusika kuwadhalilisha wanafunzi kijinsia.

Walimu kadhaa wamekuwa wakifikishwa mahakamani na wengine kusimamishwa kazi. Mwezi April 2013, mwalimu wa sekondari huko Magharibi mwa Kenya alifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kulawiti mwanafunzi mwenye umri wa miaka 19. Mwalimu huyo aliachiwa kwa dhamana na ni miongoni mwa wale waliofungiwa na tume ya huduma ya walimu.
Mwanzoni mwa wiki hii mwalimu mkuu huko Nyaza alikamatwa na polisi baada kumvua nguo mwanafunzi wa kike kwa sababu alivaa sketi fupi. Mwalimu huyo anaendelea kushukiliwa na poliosi.Mara nyingi kesi zimekuwa haziishi ambapo kwa kiasi kubwa hushughulikiwa na TSC mamlaka za shule. Wakati mwingine tatizo hili limekuwa likishughulikiwa kati ya wazazi na walimu.

 

Afisa wa shirika linalosimamia ustawi wa watoto nchini Kenya ambaye hakutaka jina lake litajwe, amemtaka mwendesha mashtaka wa serikali kuzichukua kesi na kuhakikisha watuhumiwa wa ngono dhidi ya watoto wadogo na wanafunzi wanapawsa kufikishwa mahakamani.

Nao Umoja wa walimu wa shule za msingi nchini Kenya umeelezea msimamo wake kwamba hawatomlinda mwanachama yeyote atakayekiuka maadili. Mwenyekiti wa muungano wa wazazi nchini Kenya Musau Ndunda ameitaka tume ya walimu kuwachunguza walimu wote ili kuzuia watoto wadogo kudhalilishwa kijinsia.

No comments:

Post a Comment