Tuesday, 16 June 2015

RAIS AL BASHIR AWASILI SALAMA SUDAN ....

Rais Omar al Bashir wa Sudan amewasili mjini Khartoum Sudan kutoka nchini Afrika Kusini.
Rais Bashir amekariri kuwa hana hatia yoyote wala hajui kwa nini mahakama ya kimatiafa ya ICC inasisitiza kumchafulia jina.
Shirika la habari ya AFP limemnukuu rais Bashir akifoka ''Allah Akbar'' aliposhuka kutoka kwa ndege iliyombeba.
Aidha aliinua mkongojo wake juu na kushangiliwa na wafuasi wake.
Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Ibrahim Ghandour aliwaambia waandishi wa habari kuwa serikali ya Afrika Kusini ilikuwa imemkariria rais Bashir kuwa kuwepo kwake mjini johannesburg ilikuwa ni tukio la kushabikiwa na lenye heshima kubwa kwa hivyo hakukuwa na uwezekano wowowte wake kukamatwa.
Ndege iliyombeba rais Bashir ikiondoka Afrika Kusini
Rais Huyo alikuwa ameratibiwa kuhutubia umma lakini kinasa sauti kikaharibika na akaondoka.
Rais Bashir aliingia katika gari lake lililo wazi na akaondoka uwanjani huku akishangiliwa na wafuasi wake.
Kuondoka kwake nchini Afrika Kusini kulikumbwa na hati hati, baada ya mahakama moja kuamuru rais huyo asiondoke nchini humo hadi mahakama hiyo itakaposikiliza kesi na kuamua iwapo atakamatwa na kupelekwa mjini the Hague Uholanzi au la.
Awali mwandishi wa BBC aliyeko Afrika Kusini Nomsa Maseko, alisema kuwa ndege ya rais al Bashir ilijazwa mafuta jana usiku na kuwekwa mstari wa mbele tayari kabisa kuondoka katika uwanja wa ndege wa kijeshi.
Rais Bashir alipotua mjini Khartoum
Rais Bashir aliondoka licha ya kuwepo amri ya mahakama ya kumzuia kuondoka nchini humo hadi kesi dhidi yake itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Mahakama hiyo ilikuwa inapaswa kuamua ikiwa Bwana al-Bashir atakabidhiwa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC yenye makao yake mjini Hague Uholanzi ilikukabiliana na mashtaka ya uhalifu wa kivita na mauaji yahalaiki yanayomkabili .

Majaji watatu waliokuwa wanasikiza kesi hiyo dhidi yake wamemtaka waziri wa usalama wa ndani nchini humo kueleza ni vipi rais Bashir aliruhusiwa kukaidi amri ya mahakama .

No comments:

Post a Comment