Mkurugenzi mkuu wa Twitter, Dick
Costolo, ana nia ya kujiuzulu ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Juni,
kufuatia shinikizo kutoka kwa wawekezaji, ambao wanalalamikia ukuaji
polepole wa mtandao huo wa kijamii.
Mwanzilisho mwenza wa mtandao huo Jack Dorsey atachukua mahala pake kama kaimu afisa mkuu kuanzia Julai mosi na kukalia wadhfa huo hadi pale mrithi wake atakapochaguliwa.
Bwana Costolo amekuwa akishinikizwa kujiuzulu na wawekezaji ambao hawafurahikii ukuwaji wa kampuni hiyo.
Katika taarifa yake bwana Costolo amesema kuwa anafurahishwa na wafanyikazi wa kampuni hiyo.
Mnamo mwezi Aprili kampuni hiyo ilipata hasara ya dola milioni 162.
Bei ya hisa zake ilishuka kwa asilimia 30 na sasa zinaendelea kuuzwa kwa bei ya uanzilishi wake mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment