Wednesday, 24 June 2015

SERA JUU YA MATEKA KUBADILISHWA MAREKANI ...!

 
 RAIS WA MAREKANI : BARACK H. OBAMA

Rais wa Marekani Barack Obama ametoa tamko la kubadilishwa kwa sera za nchi yake katika masuala ya kubadilishana ama kuwakomboa mateka ambao ni raia wake.

Rais ametiulia mkazo kauli yake, amesema kwamba seriakali yake haitafanya makubaliano yoyote yenye lengo la kuwakomboa mateka ambao ni raia wa Marekani waliotekwa ughaibuni,lakini aliweka bayana juu ya familia ambazo huamua kulipa fidia ya ndugu zao mateka kwamba hawatakabiliwa na mashtaka.

Rais Obama ameeleza kuwa anatambua wazi kuwa familia za mateka huwa wanachaganyikiwa pindi wanapo shughulika na serikali yao wenyewe.

Ameelezea pia mipango ya baadaye ya serikali yake na sera za nchi hiyo kwamba
kutakuwa na utaratibu maalum kiserikali kuratibu jitihada za vitengo mbali mbali na taasisi zingine zinazojitahidi kuwaokoa mateka ambao ni raia wa Marekani .Ahadi ya Rais Obama kwa raia wake ni kuchukua hatua stahiki kuwarejesha raia wake nyumbani na kuwachukulia hatua watekaji wao.

Ujumbe wangu kwa kila raia wa Marekani ambaye anashikiliwa mateka popote ulimwenguni,ni huu Marekani haitaacha kuhakikisha unaungana na familia yako.hatutasita,hata kama itatuchukua muda mrefu kiasi gani.

No comments:

Post a Comment