Serikali ya Ufaransa sasa imemtaka
balozi wa Marekani nchini humo kufika mbele yake kufuatia madai kwamba
Marekani iliwachunguza watangulizi wake wawili.
Bwana Hollande ameitisha kikao cha dharura na kusema Ufaransa haitavumilia vitendo ambavyo ni tishio kwa usalama wake.
Hatahivyo Marekani imesema kuwa haitatoa tamko kuhusu madai fulani ya kiintelijensia.
Ned Price ambaye ndio msemaji wa Baraza la kitaifa la usalama nchini Marekani ameongozea kwamba Marekani hailengi na wala haitalenga mawasiliano ya Hollande.
Shirika la NSA lilishtumiwa kwa kumpeleleza kansela wa Ujerumani Angela Merkel pamoja na viongozi wa Brazil na wale wa Mexico.
No comments:
Post a Comment