Tuesday, 16 June 2015

WALIOKUFA KWA UGONJWA WA MERS KOREA WAFIKIA 18 ....

 
Korea Kusini imesema watu watatu wamefariki duniani kutokana na ugonjwa wa Middle East Respiratory Syndrome au MERS na kufikisha idadi ya watu 18 waliokufa kutokana na ugonjwa huo.
Zaidi ya watu mia na hamsini wamegundulika kuambukizwa ugonjwa wa MERS, huku wizara ya afya nchini humo ikitangaza wagonjwa wapya wanne Jumanne.

Mlipuko wa MERS ulioanza mwezi Mei ni mlipuko mkubwa zaidi kuwahi kutokea nje ya Saudi Arabia.

 
Watoa huduma za afya nchini Korea Kusini wakijikinga na maambukizi ya ugonjwa wa MERS uliosababisha vifo vya watu 18

No comments:

Post a Comment