Kiongozi mkuu wa kundi la umoja wa ulaya Jeroen Dijsselbloem amesema kwamba ombi la hivi karibuni la Ugiriki limefanya msingi mzuri wa mpango wa misaada ya kifedha na mahitaji ya haraka ya Athens.
Mwandishi wa BBC wa masuala ya uchumi Dijsselbloem amesema mjini Brussels kwamba mkutano huo ni wenye mafanikio tangu wakati wa serikali yenye mrengo wa kushoto ilipoingia madarakani mjini Athens.Waziri wa uchumi wa Ugiriki Giorgios Stathakis amesema kwamba ombi la hivi karibuni pamoja na ongezeko la ushuru katika masuala ya biashara na utajiri ,ni wakati ambapo juhudi zinafanywa kuepusha zoezi linaloendelea la ukataji mafao ya wafanyakazi kutoka katika mishahara yao.
Wakati hayo yakiendelea Ujerumani imekataa kuidhinisha ombi la Ugiriki ,na kusema kwamba muda unahitajika kuliangalia suala hilo kwa kina.Mkutano ujao ndiyo utakao amua hatma ya uchumi wa Ugiriki.
No comments:
Post a Comment