Benki ya Ulaya imekubali kuidhinisha fedha zaidi za hali ya dharura kwa benki za Ugiriki.
Ombi lilitolewa baada ya watu wengi kutoa pesa nyingi kiasi kwamba jumla walizotoa zilifika yuro bilioni tatu juma hili pekee.Wenye akaunti nchini Ugiriki wanaogopa kuwa taifa lao litachelewa kulipa madeni na pesa zao zibadilishwe kuwa sarafu za nchini badala ya Yuro yenye thamani kubwa zaidi.
Ingawa Benki Kuu ya Ulaya imekubali kukopesha benki za Ugiriki pesa taslimu lakini itafanya hivyo tu hadi Jumatatu wakati ambapo viongozi wa kitaifa wa Jumuiya ya Ulaya watakutana.
Viongozi hao wataamua iwapo wataipa Ugiriki pesa nyingine za matumizi ambazo zimecheleweshwa kutokana na sintofahamu kati ya taifa hilo na mataifa na mashirika yanayoidai Ugiriki.
No comments:
Post a Comment