KOBE
Jeshi la Polisi, Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNAI), linamshikilia, raia wa Kuwait, Hussein Mansoor, kwa kukutwa na kobe hai 173 aliokuwa akiwasafirisha kueleka nchini kwake.
Kaimu Mkurugenzi wa Uwanja wa JNIA, Clemence Jingu
alisema abiria huyo mwenye hati ya kusafiria yenye namba 003870237,
alikamatwa usiku wa kuamkia jana akijitayarisha kupanda ndege ya
Emirates iliyokuwa ikielekea Kuwait kupitia Dubai.
Jingu alisema raia huyo alikamatwa saa tano usiku
katika eneo la abiria wanaoondoka, baada ya polisi wa JNIA kwa
kushirikiana na maofisa wa Wizara ya Maliasili kufanya ukaguzi na
kugundua kobe hao wakiwa wamefichwa kwenye masanduku makubwa mawili.
“Hii ni moja ya kazi kubwa ambazo tunazifanya kwa
sasa hapa JNIA, ila tutahakikisha kuwa hakuna nyara za Serikali
zitakazotaifishwa na kupitishwa hapa kwa kuwa tumeimarisha ulinzi
maradufu,” alisema Jingu.
Jingu alisema kobe hao wenye thamani ya Sh 30
milioni ni miongoni mwa nyara muhimu za Serikali ambazo zimekuwa
zikitaifishwa kupitia mbinu mbalimbali.
“Pamoja na kuimarisha ulinzi, lakini tutahakikisha
JNIA inakuwa bora kuliko viwanja vingine vya Afrika Mashariki na zaidi
hasa kuhakikisha ulinzi unapewa kipaumbele” alisema.
Kamanda wa Polisi wa JNIA, Khamis Suleiman,
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa huyo
anashikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi.
Tukio hilo lilithibitishwa pia na Kamishna wa
Interpol, Tawi la Tanzania, Gustav Babile ambaye alisema raia huyo
alikamatwa na wanyama hao huku akiwa na vibali halali.
Mmoja wa wafanyakazi wa JNIA (jina linahifadhiwa)
alisema kabla ya kukamatwa, ilionekana kuna mpango umefanywa ili
kumpitisha raia huyo bila kugundulika kwani taa za eneo la ukaguzi
zilizimwa kwa saa kadhaa uwanjani hapo.
“Si kawaida taa kuzimwa lakini wakati yeye anapita
taa zilizima jambo linaloonyesha kuwa ni njama zilizopangwa lakini hata
hivyo hazikufanikiwa,” kilisema chanzo hicho.
Kadhalika chanzo hicho kilisema raia huyo
aligunduliwa na askari wa maliasili akiwa tayari ameshapita katika
vizuizi vyote vya ukaguzi na ameshaingia katika eneo la abiria
wanaoondoka.
Tukio hili linafanana kwa kiasi kikubwa na lile
lililotokea Januari 8, mwaka huu, ambapo raia mwingine wa Kuwait, Ahmed
Ally Mansour alikamatwa uwanja wa JNIA akiwatorosha kenge hai 149 wenye
thamani ya Sh 6.3 milioni.
Kama ilivyo kwa tukio la jana, hata tukio la Januari lilitokea
saa tano, likihusisha ndege ile ile huku watuhumiwa wakiwa na ubini
unaolandana.
Kadhalika, Julai 31 mwaka jana, raia wa Vietnam,
Dong Van (47) naye alikamatwa uwanjani hapo akiwa na meno 65 na kucha
447 za simba zenye thamani ya Sh189.4 milion
No comments:
Post a Comment