Wakati
wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’
wanakutana leo kwenye hotel ya Tansoma kuzungumza na kocha wao mpya,
kiungo wa Simba SC na timu ya Taifa Jonas Mkude leo yeye anakwea ‘pipa’
na kutimkia Afrika Kusini kwenda kufanya majaribio kwenye klabu ya Wits
University inayoshiriki liki kuu ya nchini humo
Afisa habari wa klabu ya Simba
Hajji Manara amesema, Simba wamempa baraka zote kiungo huyo licha ya
kuwa ameitwa kwenye timu ya Taifa, Manara amesema tayari wamezungumza na
kocha wa Stars Boniface Mkwasa kumpa taarifa hiyo ya kiungo wao
anaekwenda kufanya majaribio ya siku 14 (wiki mbili).
“Tumempa baraka zote za kwenda
kufanya ‘trial’ lakini kumalizana naye ni mpaka hapo badae atakapofuzu
lakini tumempa baraka zote ‘full’, amepata ‘support’ ya Simba”, amesema
Manara.
“Ni kweli Mkude ameitwa kwenye
timu ya Taifa lakini Mungu jaalia tumeshazungumza na coach Charles
Boniface Mkwasa na kumpa taarifa hiyo kwamba Jonas anaondoka na yeye
alikuwa hana taarifa hiyo lakini nadhani haitakuwa tatizo kwake
kwasababu anachoenda kukifanya pia ni nsehemu ya ‘program’ za TFF,
lazima tuongeze ‘professionals’ wengi zaidi nadhani ni baraka kwa nchi,
wal Boniface hatakuwa na shida, ni mwalimu mweledi sana”, ameeleza.
No comments:
Post a Comment