Wednesday, 24 June 2015
YA KI' NEGA NA MANZIAKE' Mh. J. MBILINYI MBUNGE WA MBEYA MJINI NA MKE WAKE (X )
Baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’ kushinda kesi mahakamani ya kutaka apewe amlee mtoto wake aitwaye Sasha,aliyekuwa mzazi mwanzake,Faiza Ally amefunguka kuwa ni bora kufa kuliko kumuona mtoto wake akilelewa na mama mwingine wakati yeye yupo hai.
Sugu alimfikisha mahamakani mzazi mwenziye kwa madai kuwa ameshindwa kumlea mtoto wao kwa kuwa mama huyo si mwadilifu.
Faiza ameandika hivi kupitia Akaunti ya Instagram:
Sielewi joseph ameshindaje kesi- ushahidi wa picha peke yake sioni kama unatosha mimi kupokonya mtoto wangu- mtoto wangu ni mdogo sana ananihitaji sana – na sita rudi hata ikibidi kuuza kila nilicho nacho kwa ajili ya kusimamia hili- sijapewa nafasi nimepelekwa mahakamani ijumaa na leo jumanne nimepewa hukumu/ mwanangu achukuliwe….. hapana !
Sitarudi nyuma na haitakua rahisi ninakata rufaa na kutafuta wakili wa kunisimamia hili- mwanangu anasoma vizuri anaishi vizuri na naamini kwenye mikono yangu yuko salama zaidi ya kokote/ yaani kuhusu kukosa kukaa na mwanangu ni bora kufa kuliko kuishi nikimuona sasha ana lelewa na mama mwingine ikiwa mimi mama yake niko hai na makini katika malezi ya mtoto wangu- nina ndoto na mwanangu nyingi sana – nahitaji kuishi nae yeye ndio kila kitu kwenye maisha yangu/ nampenda sana mwanangu na sijashindwa kumlea- naona uchungu sana kupelekea mahakani na kupokonywa mtoto wangu bila sababu za msingi .
Sitaogopa cheo chake cha ubunge kamwe- ntasimama kama mama mwenye haki kwa mtoto wake …mungu naomba nielekeze.nisimamia na unihukumie huu ukatili ninao fanyiwa na baba Sasha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment