Friday, 19 June 2015

KISHINDO CHA Hon. E . LOWASSA KWENYE KUSAKA WADHAMINI NA ZIARA ZAKE .. HAVIKAMATIKI HATA KWA MBALI ..

 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza na Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro jana Juni 18, 2015, baada ya kudhadhaminiwa kwa kishindo na WanaCCM hao, ili aweze kupata ridhaa ya Chama chake katika kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 33,780.
 
 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za wanachama 33,780 wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, waliomdhani ili aweze kupata ridhaa ya Chama chake katika kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Anaekabidhi fomu hizo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Mjini, Loth Ole Nesele.
 
 
   
 
Umati wa wanaCCM wa Mkoa wa Kilimanjaro, ukimshangilia kwa furaha, Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani) wakati alipopanda jukwaani kuwashukuru wa kumdhamini kwa kishindo. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 33,780.
 
Ujumbe wa Vijana kwa Lowasa.

No comments:

Post a Comment