Mtandao wa Wikileaks umechapisha nyaraka
zinazoonyesha kuwa chombo cha upelelezi cha Marekani NSA kimemchunguza
rais wa Ufaransa, Francois Hollande, na marais wawili waliokuwa kabla
yake.
Inaaminika kwamba
upelelezi huo umefanyika kati ya mwaka 2006 na 2012. Idara ya Marekani
haikuweza kuthibitisha usahihi wa nyaraka hizo.
Mwandishi wa BBC
aliyopo mjini Washington amesema kuwa upelelezi uliofanywa kwa viongozi
wa Ujerumani, Brazil na Mexico ndio wa hivi karibuni zaidi
kufanyika.Moja wapo ya mazungumzo ya simu yaliyochunguzwa ni yale
yanayomwonyesha rais Hollande akiidhinisha kufanyika kwa mikutano ya
siri mapema hapo mnano mwaka 2012 kuhusu madhara ya kujitoa kwa Ugiriki
katika Umoja wa Ulaya.
James Woolsey amewahi kuwa mkurugenzi wa
shirika la ujasusi la Marekani CIA.Amesema kwa nchi kuchunguza washirika
wake ni jambo linalokea sana na hasa linahusishwa na masuala ya
kiuchumi:
"sitapenda kumtuhumu mtu yeyote kuhusiana na Ufaransa
lakini kuna baadhi ya nchi ambazo zinatumia taarifa zao za
kiintelijensia kuchunguza kuhusu utuaji wa mikataba kimataifa ili
kusaidia mashirika ya nchi zao, kusaidia hayo mashirika kutoa hongo kwa
wengine ili mashirika ya nchi zao yapewe mikataba. Watakaposita kutoa
hongo, basi na sisi tutaacha kuchunguzana."
No comments:
Post a Comment