TOKA GP ... wameandika
DOKTA Chale ambaye anaandika makala za afya katika gazeti ndugu la hili la Ijumaa, ameanika chanzo cha mastaa wengi kupata ugumba ambapo pamoja na vyanzo vingine, ameyataja madawa ya kuongeza maumbile ya mwili na ya kujichubua yanasababisha tatizo hilo.
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
Akizungumzia madawa hayo pasipo kuyataja majina (yamezagaa mitaani), dokta Chale alisema baadhi ya madawa hayo yana kemikali ambazo hupenya hadi kwenye figo na kuzisababishia madhara ambapo moja kwa moja hawezi tena kupata mtoto.Alisema amekuwa akisikia kila kukicha katika vyombo vya habari mastaa wakijieleza kuwa wamehangaika sana kupata watoto lakini imeshindikana pasipo kujua madawa hayo ndiyo chanzo hivyo ni vyema wakachukua tahadhari.
“Kwa wale ambao bado hawafikirii kuzaa ni vyema wakawa makini na madawa haya ya kuongeza maumbo yao. Yanaathiri figo na zikishaathirika mwanamke hawezi tena kupata ujauzito.
“Ni vyema wakawaona madaktari kwa ajili ya ushauri kabla hawajaanza kuyatumia maana baadhi ya dawa hizi zinaingizwa nchini bila kukaguliwa kama zinafaa kwa matumizi ya binadamu,” alisema Dokta Chale.
Miongoni mwa mastaa ambao wamesharipotiwa kuwa na tatizo la kukosa watoto kwa muda mrefu ni pamoja na mbunge mtarajiwa, Wema Sepetu ‘Madam,’ Judith Wambura ‘Jide,’ Rehema Chalamila ‘Ray C’ (pichani), Mainda Suka, Jacqueline Wolper na Jokate Mwegelo ‘Kidoti.’
No comments:
Post a Comment