Papaa Msofe akiwa mahakamani. (Picha kutoka maktaba yetu)
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imemfutia kesi
ya mauji iliyokuwa ikimkabili mfanyabishara maarufu nchini, Marijan
Abubakar, maarufu kama 'Papaa Msofe' baada ya kupokea taarifa kutoka kwa
MKurugenzi wa Mashitaka (DPP), Biswalo Mganga leo kuwa hana nia ya
kuendelea kumshitaki tena.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya
Jinai ya mwaka 2002, inampa mamlaka DPP kuifuata kesi ya jinai bila
kuhojiwa na mtu yeyote wala mamlaka yoyote ile.
No comments:
Post a Comment