Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam(hawapo pichani)wakati wa kutangaza ubora wa elimu ya ufundi inayotolewa na baraza hilo.Baraza hilo limevifuta usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.Kushoto ni Mkurugenzi wa Mitaala wa baraza hilo Twilumba Mponzi na Msaidizi wa katibu Mtendaji Alex Nkondola.
HOTUBA YA KAIMU KATIBU MTENDAJI WA BARAZA LA
TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE) DKT ADOLF B. RUTAYUGA KUHUSU TAMKO LA
BARAZA LA KUVIFUTIA USAJILI BAADHI YA VYUO NA KUVISHUSHA HADHI VINGINE -
24/06/2015
Ndugu Waandishi wa Habari
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, kwa lengo la kusimamia na kuratibu taaluma zinazotolewa na taasisi na vyuo vva elimu ya ufundi nchini, ambavyo siyo vyuo vikuu au vyuo vikuu vishiriki. Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini kwa kusimamia kikamilifu shughuli za kuendesha mafunzo ili tuzo zinazotolewa na taasisi na vyuo ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa.
Kwa kutumia Sheria na Kanuni za Baraza za Usajili (2001) na zile za Ithibati na Utambuzi (2001), mnamo tarehe 20 Februari 2015, Baraza lilitoa notisi ya siku 30 kwa taasisi na vyuo vilivyokiuka taratibu na vyenye mapungufu makubwa ya Usajili na Ithibati kupitia taarifa yake kwa Umma. Notisi hii ililenga kuzipa taasisi na vyuo nafasi ya kujirekebisha.
Baraza linakiri kuwa taasisi na vyuo vingi kama vilivyoorodheshwa kwenye Jedwali Na. 1, Jedwali Na. 3, na baadhi kwenye Jedwali Na. 5 vimechukua hatua mbalimbali za kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza. Hata hivyo, hadi kufikia leo tarehe 24 Juni 2015 yaani siku 124 baada ya Notisi ya Baraza, kuna vyuo ambavyo havijachukua hatua yoyote ya kurekebisha mapungufu yake kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 2 na Jedwali Na. 4.
Tamko la Baraza
Kutokana na mapungufu hayo Baraza limeamua kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zake kwa taasisi na vyuo vyote vilivyoorodheshwa katika Jedwali Na. 2 na Jedwali Na. 4 kwa makosa yafuatayo:
a) Ama kumalizika kwa muda wa Usajili wa Awali (Preparatory Registration) na Usajili wa Muda (Provisional Registration); au
b) Kutoanza mchakato wa kupata Ithibati baada ya kupata Usajili Kamili; au
c) Kumalizika kwa muda wa Ithibati na kutochukua hatua ya kuomba upya Ithibati (re-affirmation); na
d) Taasisi na Vyuo kuamua vyenyewe kusitisha kutoa mafunzo kwa sababu mbalimbali.
No comments:
Post a Comment