Monday, 22 June 2015
KOMBE LA DUNIA WANAWAKE .. UINGEREZA NA MAREKANI WATINGA ...
Marekani imefanikiwa kuingia katika robo fainali za kombe la dunia wanawake jumatatu usiku baada ya kuifunga Colombia 2-0 katika mechi iliyochezwa Montreal, Canada.
Marekani sasa itakutana na China katika mechi ya robo fainali siku ya Ijumaa.
Katika mechi nyingine ya Jumatatu usiku Uingereza, nayo ilifanikiwa kuingia robo fainali kwa kuifunga Norway 2-1 na sasa itakumbuna na wenyeji Canada katika robo fainali Jumamosi.
Ujerumani inakumbana na Ufaransa, katika robo fainali nyingine wakati Australia, inasubiri mshindi katika mechi ya Uholanzi, na Japan, itakayochezwa hivi leo.
Katika mechi ya Marekani, na Colombia, Alex Morgan, aliipatia marekani bao la kwanza katika dakika 53 na Lloyd, akafunga kazi kwa bao la pili kwa njia ya penalty katika dakika ya 65.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment