Watoto wapatao 48 wameokolewa katika mashamba ya Kakao walikokuwa wakitumikishwa kusini Magharibi mwa Ivory Coast.
Shirika la Kimataifa la Polisi la Interpol limesema pia limewakamata wafanyabiashara wa magendo 22.Watoto hao wenye miaka kuanzia mitano mpaka 16, wametoka Burkina Faso, Guinea, Mali na pia kaskazini mwa Ivory Coast.
Shirika hilo limesema baadhi ya watoto walikuwa wakifanya kazi katika mashamba hayo kama watumwa wakiwa na hali mbaya, bila ya malipo wala kusoma shule.
Polisi mia mbili nchini Ivory Coast walishiriki katika operesheni hiyo ya uokozi, iliyoratibiwa na Interpol pamoja na Shirika la Kimataifa la Wahamiaji (IOM).
Operesheni hiyo ni ya kwanza ya aina yake katika nchi za Afrika magharibi na maeneo mengine.
No comments:
Post a Comment