war pic.
Waraka huo wenye kurasa 9 unaozagazwa na chama hicho, unawataka wafuasi wa chama tawala kuwatambua maadui wa utawala na kujitenga nao. Chama hicho kimewataka wafuasi wake kuichukulia miungano wa vyama vya upinzani, Adc-Ikibiri, Ranac Dushayure Uburundi bwogorore, baadhi ya mashirika ya kiraia na vituo vinne vya redio za kibinafsi: RPA, Bonesha fm, Isanganiro pamoja na redio na televisheni Renaissance fm.
Katika waraka huo chama cha Cndd-Fdd kimevinyooshea kidole vituo vya redio hizo za kibinafsi, baadhi ya mashirika ya kiraia, na upinzani kwamba walihusika katika vita viliyotokea mwishoni mwa mwaka uliyopita katika mkoa wa cibitoke, kaskazini magharibi mwa Burundi. Chama hicho kimewasihi wafuasi wake kutounga mkono upinzani, mashirika ya kiraia na vituo hivyo vya redio za kibinafsi, kwani vinaundwa na kabila tofauti na wao.
Kiongozi wa chama cha Cndd-Fdd katika mkoa wa Bubanza, Juvénal Havyarimana, amekiri kuwa chama tawala cha Cndd-fdd, ndio kimeandika waraka huo.
Mwenyekiti wa muungano wa vyama vya upinzani Adc-Ikibiri, Léonce Ngendakumana amesema hana muda wakuzungumzia waraka huo, kwani chama cha Cndd-Fdd, kinataka kuwapotezea muda ili wasiendelea kujiandalia uchaguzi.
Kwa upande wake, Mbunge Jean Minani, akiwa pia kiongozi wa chama cha Sahwanya-Frodebu Nyakuri, moja ya vyama vinavyounda mmungano wa vyama vya upinzani Ranac, amesema wako mbioni kukifungulia mashitaka chama cha Cndd-Fdd kutokana na uchochezi wa kikabila.
Naibu mwenyekiti wa shirika la redio nchini Burundi (ABR), Patrick Nduwimana, amewataka raia kutoshawishiwa na waraka huo, huku akilani mafunzo hayo, ambayo aliyaita potovu. Mafunzo ambayo yanalenga kuleta ubaguzi kati ya raia, amesema Nduwimana.
Katika hotuba yake wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 24 ya Umoja wa Warundi, rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, alibaini kwamba kuna mashirika ya kiara ambayo yanaundwa na kabila moja, akiyataka kujirekebisha, jambo ambalo linaendelea kuleta mvutano kila kukicha nchini Burundi.
Hayo yanajiri wakati ikisalia miezi 3 ili uchaguzi mkuu ufanyike.

No comments:
Post a Comment