Wednesday, 11 February 2015
WATU 300 WAFA MAJI MEDETERRENIA
Wahamiaji wasiopungua 300 waliojaribu kuvuka bahari ya Mediterrania katika baridi kali wakiwa kwenye maboti ya wazi ya mipira, Wameripotiwa kutojulikana walipo na manusura, huku shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa na makundi mengine ya misaada wakiiosoa vikali operesheni mpya ya Umoja wa Ulaya, kwa kutokidhi mahitaji na kugharimu maisha. Wahamiaji hao wanaoshukiwa kuwa wamefariki, wanaongezea kwenye idadi ya vifo vingine 29 vilivyoripotiwa mapema wiki hii na kikosi cha askari wa pwani wa Italia.
Kamishna mkuu wa wakimbizi wa Umoja wa Mataifa amesema manusura waliripoti kwamba boti nne ziliondoka pamoja, bila chakula wala maji, na kwamba ziliondoka karibu mara moja. Karibu watu 107 waliokolewa na askari wa ulinzi wa pwani wa Italia na meli ya uvuvi. Utaifa wa manusura na wale wasiojulikana walipo haukuweza kutolewa mara moja, lakini idadi kubwa ya wanaowasili kwa wakati huu wanakimbia migogoro nchini Syria, Iraq, Mali na kwingineko
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment