Friday, 13 February 2015

DENI LA MAN U LAONGEZEKA .. >>

 
Mapato ya matangazo ya kilabu ya Manchester United yameshuka kutokana na timu hiyo kukosa kushiriki katika ligi ya vilabu bingwa ulaya.

Kulingana na makadirio ya fedha ya kilabu hiyo, deni lake limepanda hadi pauni millioni 24 katika kipindi cha miezi mitatu.

Naibu afisa mkuu Ed Woodward hatahivyo amesema kuwa mkataba mpya wa maonyesho ya mechi za ligi hiyo pamoja mapato mazuri ni ishara kwamba bado wapo katika nafasi nzuri.

Mapato ya matangazo yalishuka kutoka pauni millioni 46.9 katika kipindi kama hicho msimu uliopita hadi pauni millioni 28.4 ambayo ni aslimia 39.4 huku mapato yanayopatikana wakati wa mechi yakishuka kutoka pauni millioni 33.7 hadi pauni millioni 30.9.

No comments:

Post a Comment