Mboni Mhita UVCCM ...
Ahsantee ! bwana MAKONDA ( free pass )
Anaetajwa kupanda chati kwa kumtusi LOWASSA ...
Dodoma. Rais Jakaya Kikwete ametengua uteuzi wa wakuu wa wilaya 12 na kuwateua wengine 27, akiwamo aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen na mjumbe wa Bunge la Katiba, Paul Makonda ambaye aliingia kwenye mzozo na mawaziri wakuu wawili wa zamani.
Katika uteuzi huo uliotangazwa jana na Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda mjini hapa, katibu mkuu wa zamani wa Shirikisho la
Soka (TFF), Frederick Mwakalebela ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Wanging’ombe, huku wakuu wa wilaya 64 wakibadilishiwa vituo vyao vya
kazi.
“Mabadiliko haya yamezingatia kuwapo nafasi 27
wazi zinazotokana na kufariki dunia kwa wakuu watatu wa wilaya, watano
kupandishwa vyeo kuwa wakuu wa mikoa, saba kupangiwa majukumu mengine na
12 kutenguliwa uteuzi wao. Wakuu wa wilaya 42 wamebaki katika vituo
vyao,” alisema Pinda wakati akitangaza uteuzi huo.
Pinda alitangaza uteuzi huo jana alasiri na baadhi
ya wakuu wa wilaya ambao walibadilishiwa vituo walishangazwa na taarifa
za uhamisho huo, ambao umeelezewa na viongozi wa vyama vya upinzani
kuwa ni wa kufuja fedha za walipa kodi na unalenga kukiandaa chama hicho
kwa Kura ya Maoni na Uchaguzi Mkuu ujao.
“Yaani unanipongeza kwa nini?... mimi
nimehamishwa? Nimehamishiwa wapi?” alihoji mmoja wa wakuu wa wilaya
baada ya kupigiwa simu na Mwananchi, lakini akaomba asitajwe gazetini.
Katika uteuzi huo yumo Zelotte, ambaye ni kati ya
maofisa wachache wa Jeshi la Polisi kuteuliwa kushika nafasi za ukuu wa
wilaya na hivyo atalazimika kuacha kibarua cha fani yake na kwenda
Musoma. Zelotte anasifika kwa kufanikiwa kukamata vijana 11 waliokuwa
wakihusishwa na mazoezi ya kigaidi mkoani Mtwra mwaka 2013.
Pia yumo Makonda, ambaye ameteuliwa kuwa mkuu mpya
wa Wilaya ya Kinondoni. Kiongozi huyo wa Umoja wa Vijana wa CCM
aliandikwa sana na vyombo vya habari wakati wa Bunge la Katiba kutokana
na kutoa maneno ya kumshambulia mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba aliyewasilisha Rasimu ya
Mabadiliko ya Katiba.
Kiongozi huyo wa UVCCM aliandikwa zaidi na vyombo
vya habari kutokana na kuhusishwa na vurugu zilizotokea Hoteli ya Blue
Pearl jijini Dar es Salaam wakati wa mdahalo wa Katiba Inayopendekezwa
akidaiwa kumshambulia mwilini Warioba, ambaye amewahi kuwa Waziri Mkuu
na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, makada wawili wa CCM,
John Guninita na Mgana Msindai walimwandikia kusudio la kumfungulia
mashtaka wakidai kuwa Makonda aliwadhalilisha kwa kuwaita kuwa vibara wa
Edward Lowassa, ambaye ni mbunge wa Monduli na aliwahi kuwa Waziri
Mkuu.
Makonda aliwahi kuitisha mkutano na waandishi wa
habari na kumtuhumu Lowassa akidai kuwa anawatuma baadhi ya makada wa
chama hicho wanaokivuruga chama. Alidai kuwa Lowassa hawezi kuwa Rais wa
Tanzania na kwamba CCM haitafuti Rais pekee, bali mwenyekiti wake na
mbunge huyo wa Monduli hawezi kuongoza chama hicho kikongwe.
Waliotenguliwa
Ma-DC waliotenguliwa ni pamoja na Martha Umbulla
aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Kiteto, ambayo imekithiri kwa migogoro ya
ardhi kati ya wakulima na wafugaji. Mgogoro huo umesababisha watu zaidi
ya 10 kuuawa na wengine kujeruhiwa.
No comments:
Post a Comment