Watu watatu wamejeruhiwa baada ya
kutokea kwa mlipuko wa guruneti katika mgahawa mmoja mjini Mandera, kaskazini
mashariki mwa Kenya
Mlipuko huo
ulitokea Alhamisi jioni wiki hii, kwa mujibu wa taarifa za polisi, na majeruhi
hao wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya mji wa Mandera.
Job
Boronjo, Kamanda wa polisi katika Kaunti ya Mandera ameliambia Gazeti la kila
siku nchini humo kwamba polisi wanatafuta watu waliohusika na urushaji wa
guruneti hiyo.
Mkuu huyo
wa polisi katika Kaunti ya Mandera ameongeza kuwa maafisa wake wako makini
kutokana na vitisho vya kundi la Al Shabab kutoka nchini Somalia kuendelea
kutishia kutekeleza mashambulizi katika eneo hilo.
Haya ndio
mashambulizi ya haivi karibuni kuripotiwa katika eneo hilo karibu na Somalia,
na yanakuja wakati huu walimu wanaofanya kazi katika Kaunti hiyo wakiendelea
kususia kurudi kazini kwa hofu ya usalama.
Mwaka jana,
mashambulzi mawili yaliyokea katika Kaunti hiyo ya Mandera baada ya abiria 28
kuuawa katika mashambulizi yaliyoendeshwa na Al Shabab wakiwa njiani kwenda
jijini Nairobi na wachimba migodi 36 kuuawa baada ya kuvamiwa na kushambuliwa.
No comments:
Post a Comment