Thursday, 12 February 2015

JESHI LA CAMEROON KWENYE MPAKA WA NIGERIA ...>>

 Kikosi maalumu cha wanajeshi wa Cameroon, BIR, kinakabiliwa kila kukicha na mashambulizi ya Boko Haram.
Jeshi la Cameroon limekua likikabiliwa kila kukicha na mashambulizi ya Boko Haram kwenye mpaka wa Nigeria, katika mkoa wa Kaskazini. Kwa kipindi cha miezi tisa mashambulizi ya Boko Haram yameongezeka na kusababisha maafa makubwa.

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram wamekua na nguvu za hali ya juu, kundi hilo la Boko Haram likiwa na magari ya kivita na zana nzitonzito za kijeshi. Hivi karibuni mji wa Kolofata ulishuhudia mashambulizi ya kundi hilo la Boko Haram.

Ngome za kijeshi katika mji huo zililengwa na msahambulizi hayo. Shambulio lililotokea Januari 12 mwaka 2015 lililghatimu maisha ya watu wengi, na ni shambulio baya kuwahi kutokea katika mji huo wa Camerron.
tangu miezi tisa wakiwa katika vita dhidi ya Boko Haram, wanajeshi vijana wa Cameroon wamekua sasa maveterani. Vita vyao vinajulikana kwa jina la Amchidié, Achigachia au pia Kolofata.

Mji huu wa Kolofota ulishuhudia mashambulizi mengi, ikiwa ni pamoja na shambulio la Januari 12, lililogharimu maisha ya watu wengi. Siku hiyo, Djankou ambaye alikua akiongoza operesheni katika mji huo wa Kolofota dhidi ya Boko Haram, majeshi yake yalikabiliana vikali na wapiganaji wa kundi hilo la Boko Haram.

“ Ni shambulio kubwa, kwa sababu BH walikua wameapa kuuteka mji wa Kolofata na kuweka bendera yao”, ameeleza afisa huyo wa jeshi la Cameroon.
Hapa BH, ametaka kumaanisha wapiganaji wa kundi la Boko Haram

No comments:

Post a Comment